Mama Ye! leo, Mei 5, inatoa wito kwa Mh. Dk Hussein Mwinyi (MB), Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,
kushughulikia kwa haraka upungufu wa idadi ya wakunga wanaohitajika ili kuwasaidia akina mama wa
Tanzania kujifungua salama.
Wakunga wana jukumu kubwa la kuwahudumia wanawake katika kipindi chote cha ujauzito na pia ni
wataalamu wenye ujuzi wa kushughulikia matatizo yanayoweza kujitokeza wakati wa kujifungua.
Wakunga wengi wanatembea umbali mrefu na kufanya kazi masaa mengi ili watoe huduma bora kwa
wanawake katika jamii zao. Wataalamu wa masuala ya afya ya wajawazito na watoto wachanga
wamekadiria kuwa, iwapo wanawake wote wa Tanzania wangepata huduma za wakunga wenye ujuzi,
basi maisha ya akinamama wapatao 5,000 na vichanga 32,000 yangeweza kuokolewa ifikapo 2015.
Akiongea kwa niaba ya kampeni ya Mama Ye! Craig Ferla amesema: “Ni vyema kabisa kuwaenzi
wakunga wetu katika Siku ya Wakunga Duniani. Tunapongeza ahadi za serikali kuitilia mkazo sera ya
huduma za afya ya uzazi kuwa bure, lakini mengi bado yanahitaji kufanyika ili kuongeza idadi ya
wahudumu wa afya.”
Takwimu zilizochapishwa na ripoti ya Hali ya Wakunga Ulimwenguni (State of the World’s Midwives)
zinaonyesha kuwa Tanzania inahitaji wakunga 9,941 zaidi ili kufikia lengo ifikapo mwaka 2015 la kuwa na
asilimia 95% ya wajawazito wanaozalishwa na wahudumu wenye taaluma.
Craig Ferla ameongeza kuwa: “Tunawaalika na kuwahimiza Watanzania kutoa shukrani kwa wakunga –
na kusaidia kuwapa moyo vijana nao waamue kuwa wakunga siku za baadae. Unaweza kufanya hivyo
kwa kutumia ‘Twitter’ ukiwaambia asante kwa kujituma kazini, pia waweza kuweka picha kwenye
ukurasa wetu wa ‘Facebook’ zinzazowaunga mkono wakunga wetu wa Tanzania pamoja na mathalan
kutambua juhudi kubwa za mkunga unayemthamini kwa kazi zake kubwa katika jamii yako.”
Ukitaka kufahamu zaidi kuhusiana na hali ya wakunga nchini Tanzania, tembelea tovuti ya
www.mamaye.or.tz/sw ambapo utapata ushahidi uliowekwa kwa namna rahisi kuelewa, habari kuhusu
mashujaa katika uzazi salama, ahadi zilizowekwa na serikali na hatua mbali mbali unazoweza kuchukua web: www.mamaye.or.tz
twitter: @MamaYeTZ
facebook: facebook.com/MamaYeTZ
MamaYe! 164C Msasani Beach, Kinondoni,
P.O. Box 13731, Dar es Salaam, Tanzania
Phone: +255 (0) 754 588 233
ili kufanikisha kampeni hii muhimu. Ipaze sauti yako isikike na toa madai ya msingi zaidi, jiunge na
kampeni ya Mama Ye!
Uzazi wa mpango unahusu! Kama tutazaa kwa uzazi wa mpango na kulimit watoto watatu kwa kila familia hata wakunga tulionao wanatosha! Uzazi wa watoto kumi kwa familia moja na kila familia ikifnaya hivi hata tufanyeje hatufikii lengo kama watanzania, mana inatkiwa propotionality yake iendaye na namba ya wazazi kwa mkunga mmoj! Hatuwezi kufika huko hata kidogo hata wakiongezeka na wanaopewa huduma waka triple haitaleta tija. Kazi za risk watu wanakwepa kusomea hayo siku hizi kwa nchi kama Tanzania ambayo hata vifaa muhimu hakuna, mzazi anatakiwa kwenda na vifaa kama pamba , gloves anapoenda kujifungua! nani akasomee ukunga? Na hata mishahara midogo na kazi zenyewe ni ngumu na zina risk nyingi. Mabadiliko yanatakiwa kuanzia mishahara yao iwe mikubwa na risk allowances zinazoeleweka, then watu wapewe elimu ya uzazi wa mpango mana mtu anazaa mpaka anazeeka hapo ni mtoto wa 15. Mungu atusaidie, kwani challenges ni nyingi mno.
ReplyDeleteAsante mdau hapo juu. Kama ulivyosema
ReplyDelete1) wakunga wanakuwa at risk kupata magonjwa
2) mshahara mdogo
3) masaa ni mengi ya kufanya kazi
4) Vifaa hamna
5) wagonjwa wamekuwa wajuaji sana hadi kuwa na viburi
6) wakunga hawapewi appreciation kwa kazi wanazofanya
Kutokana na hizo sababu wengi hawataki kufanya kazi mawodini.
La mwisho mkiweka limit ya umri eti mwenye 50 hatumtaki basi mnakosa wengi wenye uzoefu mkubwa wa kazi.
Wakunga wapo Tanzania,isipokuwa ajira ndio hazipo labda.Mimi nina ndugu yangu Trained nurse midwife, amesubiri ajira ya serilkali zaidi ya miaka miwili sasa mpaka ameamua kufanya private hospital. Je do we real have midwives shortage?
ReplyDelete