Salaam Ankal,
Leo nimeudhiwa sana na Dereva wa Lori hili,aliekuwa ameegesha vibaya kwani alikuwa ameziba njia tena kwa makusudi kabisa,njia ambayo inaunganisha mitaa.halafu nilipomfata na kumuomba aegeshe vyema lori lake hilo ili sisi wengine tupite kwa kua njia yenyewe ni hiyo hiyo tu,alinijibu jeuri na kunitaka nifanye lolote lakini yeye hatoi gari hapo kwani ndivyo alivyoamua kupaki.kiukweli alinikera sana na kauli zake hizo,kwani alikuwa amefanya kosa kuziba njia halafu anajibu jeuri kana kwamba hii njia ni ya kwake peke yake au familia yao.
Mdau wa Globu ya Jamii.
Hebu angalieni jamaa alivyoweka gari.
naamini kauli yako ndo iliyomfanya awe na kiburi. jifunze kuwa na kauli nzuri hata kama umekosewa
ReplyDeletePole bro! Wengine huwa wanatembea na viroba kwenye hayo magari makubwa.Sasa kazi ya kiroba ikishapanda kichwani uwezo wa kufanya maamuzi ya busara hupungua sana ndio matokeo yake hayo!!!
ReplyDeletewaendesha malori wengi wanaosafiri kwenda mikoani au nchi za nje ni wastaarabu sana sana... lakini hao wa mjini, yaani wabeba michanga, maji,wahamishaji watu, wabeba mawe, n.k ni wajeuri na hawana hata adabu! nina wasi wasi sana bangi zao huwa wanavuta ili kukomesha watu barabarani!
ReplyDeleteHivi na hii tutaiita barabara? Watanzania tuamke
ReplyDeletehalafu michuzi na wenzako ndio mnatudanganya humu bloguni kila siku kuwa maisha tz yamekuwa mazuri hivyo sisi tulio first world turudi...kweli???maana inaonyesha kila kitu bado kipo shaghalabagala hakuna sheria, hakuna kuheshimiana, hakuna ustaarabu...jamaa hata kupiga simu polisi waje wamshughulikie huyo ameona atapoteza muda maana nothing will be done...sad story!
ReplyDeletemdau chicago
Did you call polis?
ReplyDeleteRudi kwenu wewe! Mkataa kwao mtumwa.Ukweli ni kwamba wengi wa mnaoaoishi ughaibuni mnapiga msuli kwelikweli kuweza kujikimu tu kwa maisha ya huko.Juhudi hizo au huo msuli mngeufanyia nyumbani mngekua mbali mno!
ReplyDeletemdau wa chicago umenena la maana
ReplyDeletekungekua na utawala wa sheria wala hili lisingetokea....kwa wanzetu hapo angeshaamrishwa kutoa lori na fine juu na akikataa angepigwa pingu papo papo na lori kulikuta na kwenda kulikomboa kituoni kwa gharama za mwenye lori
bado mimi sielewi kwa nini jeshi la polisi halitengenezi pesa ya nguvu kwa serikali....makosa mengi sana barabarani!
Nimesikitishwa sana na kauli ya mdau wa kwanza kwani hakuna kauli yeyete inaruhusu mtu kuegesha gari hivyo...actually unahaki ya kumwita jina linalofanana na kitendo alichotenda. hii ni tabia imeenea mimi aliwahi mmoja kunitemea mate wakati najaribu kumuarifu na ninaamini nilikuwa polite. nilimpeleka police nikiwa na ushahidi wa mate na mtu tulikuwa naye ktkt gari bado police walinibeza na kudai wanavitu muhimu kufuatilia sio hilo. naungana na mdau wa hapo juu kuwa nchi haina value kabisa...... polke mdau.
ReplyDeletepicha imepigwa vibaya au ni kweli sioni barabara hapo? kosa la dereva wa lorry lipo wapi sasa maana sioni barabara hapo? au ulikuwa unamaanisha amezima 'uchochoro'?
ReplyDeleteAsante.
Tuwe makini katika kutafakari mambo ukiangalia mazingira katika picha inaonyesha wazi kuwa lori lile lilikuwa pale kwa shughuli maalum ya kushusha mzigo ambapo ilibidi lisimame na kuzuia njia kwa muda na ndio maana ha ta dereva yumo garini hajashuka, ingekuwa kituko kama dereva angekuwa amekwenda maeneo yale kusalimia jamaa zake na kuegesha kama alivoegesha. ni ukosefu tu wa uvumilivu kwa aliyetuma picha na habari hii
ReplyDeleteHahahha lol pole kaka kwa kutemewa mate ! Hahahaha ! Sisi waafrica ni wanyama si binadamu kabisa
ReplyDeletehapo hamna barabara , nachoona mimi ni swimming pool .
ReplyDelete