Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Mhe. Zaipora Pangani akiongea kwenye hafla ya uzinduzi wa wiki ya maadhimisho ya wiki ya fistula leo mjini Bukoba. Wa kwanza kulia ni Balozi wa Chapa Vodacom Msanii Mwana FA na Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacam Salum Mwalim. Wengine pichani kushoto ni Mwakilishi wa CCBRT Kasper Mmuya na Katibu Tawala Mkoa wa Kagera Nassor Mnambila.Maadhimisho hayo yanafadhiliwa na Vodacom, Vodafone na CCBRT
 Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Zaipora Pangani akiongea kabla ya kukabidhi  funguo ya gari kwa Balozi wa Chapa Vodacom Msanii Mwana FA tayari kuanza safari ya kuanza Bukoba kwenda Dar salaam kupitia mikoa mbalimbali kuelimisha jamii juu ya tatizo la fistula na jinsi matibabu yanavyopatikana bila malipo katika hospitali ya CCBRT kwa ufadhili wa Vodacom. Kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera Nassor Mnambila na Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim.Kilelele cha maadhimisho hayo kitafanyika Mei 23 siku ya fistula duniani.
 Mwakilishi wa Taasisi ya CCBRT Kasper Mmuya akiongea kwenye hafla ya  uzinduzi wa wiki ya maadhimisho ya wiki ya fistula leo mjini Bukoba. Wengine pichani ni Kkatibu Tawala Mkoa wa Kagera Nassor Mnambila, Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Mhe. Zzaipora Pangani, Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim na Balozi wa Chapa Vodacom Msanii Mwana FA.Maadhimisho hayo yanafadhiliwa na Vodacom, Vodafone na CCBRT.
 Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Zaipora Pangani akikabidhi funguo ya gari kwa Balozi wa Chapa Vodacom Msanii Mwana FA tayari kuanza safari ya kuanza Bukoba kwenda Dar salaam kupitia mikoa mbalimbali kuelimisha jamii juu ya tatizo la fistula yakiwa na ujumbe fistula inatibika, jitokeza upate matibabu bila ya malipo katika hospitali ya CCBRT kwa ufadhili wa Vodacom na Vodafone ya nchoini Uingereza.
 Wakaazi wa Mji wa Bukoba waliofurika kushuhudia uzinduzi wa wiki ya maadhimisho ya wiki ya fistula uliofanywa leo mjini humo kueleka siku ya fistula duniani Mei 23. Maadhimisho hayo yanaratibiwa na kufadhiliwa na Vvodacom, Vodafone na CCBRT yakiwa na ujumbe “Fistula inatibika, jitokeza upate matibabu bila ya malipo.”
Balozi wa Chapa Vodacom Msanii Mwana FA akchana mistari kukonga nyonyo za wakazi wa mji wa Buko wakati wa uzinduzi wa wiki ya maadhimisho ya wiki ya fistula uliofanywa leo mjini humo kueleka siku ya fistula duniani Mei 23. Maadhimisho hayo yanaratibiwa na kufadhiliwa na Vvodacom, Vodafone na CCBRT yakiwa na ujumbe “Fistula inatibika, jitokeza upate matibabu bila ya malipo.”

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 18, 2013

    Kwa kweli kila mtu na kismeti chake..kwa kweli ilipendeza sana msanii amambae angeshabihiana na hii kampeni ilibidi awe wa kike, maana Fistula ndio inawaathiri wao kwa sana, ila mwanaume duhhh..kweli mambo haya ni kujuana sana...hizi ni dili tu zisizo kua na kutovaa uhusika

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 19, 2013

    Nafikiri mtoa mada hapo juu amesahau kuwa mfumo unaotawala kwa sasa na ambao wengi tunapambana kuusawazisha ni mfumo dume; sasa basi ni vyema mchawi akapewa mtoto....napongeza sana hatua hii ya kumpa MTOTO mwanaume..mwana FA...ili tatizo hili nalo liwa wazi kwa wanaume na wakiombwa fedha za vipimo..nakadhalika wawe washiriki wasiwe walalamishi..COOOL VODACOM

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...