Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Fadhili Manongi (kulia) na Mwenyekiti wa Bodi ya TCAA , Juma Mbwana Juma wakibadilishana makabrasha katika mkutano wa wazi wa siku moja wa maboresho ya utoaji wa leseni kwa makampuni mbalimbali yanayohudumia viwanja vya ndege nchini.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Fadhili Manongi (kulia) akifafanua jambo wakati wa mkutano wa wazi wa siku moja wa maboresho ya utoaji wa leseni kwa makampuni mbalimbali yanayohudumia viwanja vya ndege nchini.Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya TCAA , Juma Mbwana Juma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Alia Aviation Consultants Mahmud .M. Shamte (aliesimama) akifafanua jambo katika mkutano huo wa maboresho ya utoaji wa leseni kwa makampuni yanayohudumia viwanja vya ndege . Mei 30.2013 jijini Dar es Salaam .
Baadhi ya wadau wa mkutano wa wazi wa maboresho wa utoaji wa leseni kwa makampuni yanayohudumia viwanja vya ndege nchini wakifuatilia mada mbalimbali katika mkutano wa siku moja uliofanyika Mei 29.2013, jijini Dar es Salaam ulioandaliwa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Mkutano huo umezungumzia masuala mbalimbali jinsi ya kuboresha huduma za usafiri wa anga pamoja na changamoto mbalimbali zinazowakabili wadau wa sekta hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji kutoka Equity Aviation Services (T) Ltd Rosemary Kacungira akichangia mkutano wa wazi wa maboresho ya utoaji wa leseni kwa makampuni katika mkutano wa siku moja wa wadau wa sekta ya usafiri salama wa anga jijini Dar es Salaam Mei.29.2013.
Mwenyekiti wa LSG Sky Chefs Ltd, Paul Lyimo (aliesimama) akichangia katika kikao kazi cha wazi cha kujadili utoaji leseni kwa makampuni yanayohudumia viwanja vya ndege nchini.Picha zote na Johary Kachwamba wa MAELEZO.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...