Mkurugenzi wa Airtel Bw Sunil Colaso akiongea na wahitimu mafunzo ya mauzo na usambazaji yanayoendeshwa na Airtel Centum Sales University (ACSU) wakati wa tafrija iliyofanyika katika ofisi za Airtel makao makuu morocco. Wahitimu hao ni wafanyakazi wa Airtel Tanzania.
Mkurugezi wa mauzo na masoko wa Airtel bw Mustafa Kapasi (kushoto) akimkabidhi cheti cha kuhitimu mafunzo Afisa mauzo kanda ya dar es salaam Airtel John Gondwe baada ya kuhitimu mafunzo ya mauzo na usambazaji ya muda wa miaka miwili yanayoendeshwa na Airtel Centum Sales University (ACSU). Wafanyakazi 56 kutoka katika mikoa mbalimbali walihitimu mafunzo hayo, akishuhudia katikati ni Mkurugenzi Rasilimali watu Patrick Foya akifatiwa na Melvin Joel Meneja wa Centum Learning Makao Makuu.
Meneja Mauzo wa Airtel Bw Stratory Mushi (katikati) akiwa katika picha ya pomaja na wahitimu mafunzo ya mauzo na usambazaji yanayoendeshwa na Airtel Centum Sales University (ACSU) wakati wa tafrija iliyofanyika katika ofisi za Airtel makao makuu morocco. Wahitimu hao ni wafanyakazi wa Airtel Tanzania.
wahitimu mafunzo ya mauzo na usambazaji yanayoendeshwa na Airtel Centum Sales University (ACSU) wakikata keki kwa pamoja wakati wa tafrija iliyofanyika katika ofisi za Airtel makao makuu morocco. Wahitimu hao ni wafanyakazi wa Airtel Tanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 13, 2013

    Haya mavazi sikuhizi hayatendewi haki.....

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...