Na Abdulaziz Video,Ruangwa
Jumla ya wanafunzi 212 Kati ya 449 wanaosoma kati ya darasa la tatu
hadi la saba katika Shule za Msingi za Nandagala na Mkata Wilayani
Ruangwa, Mkoani Lindi hawajui kusoma wala kuandika huku wengine 15
ambao wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu huku
wakiwa hawajui kusoma wala kuandika.
Hayo yamebainika katika kikao cha wadau wa Elimu Wilayani Ruangwa
kilichokaa chini ya Mwenyekiti wake,Mkuu wa Wilaya hiyo Agness
Hokororo Kupokea taarifa za hali ya Elimu na kutafuta Ufumbuzi wa
chaongamoto zinakwamisha Elimu Wilayani humo kilichofanyika jana.
Wakichangia katika kikao hicho Baadhi ya Wadau wakiwemo Madiwani wa
Halmshauri hiyo walieleza kuwa Mwamko Mdogo wa Wazazi na Uwezo mdogo
wa Walimu katika Ufundishaji ikichangiwa na Upungufu mkubwa wa walimu
pamoja na Mila na Desturi ni baadhi ya changamoto zinazokwamisha
ukuaji wa Elimu Wilayani Humo.
Andrew Chikongwe,Diwani Kata ya Nandagala alisema kuwa tatizo lipo kwa
walimu kwani wengi wao hawajitumi katika ufundishaji licha ya kuwepo
kazini muda wote hali inayoonyesha kuwa wana mgomo baridi.
“Pamoja walimu kuwepo kazini lipo tatizo la kutojituma katika
ufundishaji hii inachangia sana watoto wetu wafanye vibaya”alisema
Chikongweali.
Naye Juma Nampupanga ambaye ni Mfanyabiasharaalisema kuwa kutotilia
mkazo wa elimu miongoni mwa wananchi ni kikwazo kikubwa kwa mafanikio
ya watoto wetu kwani wananchi wengi wa wilaya ya Ruangwa hawana mwamko
wa elimu kwani si kipaumbele cha hivyo kutofuatilia maendeleo ya
watoto.
Ibrahimu Ndoro Diwani wa Kata ya Ruangwa aliitaka serikali kuwachulia
hatua baadhi ya walimu wanaopangwa kufanya kazi katika Wilaya za mikoa
ya kusini ambao mara wakisharipoti huwa wanaondolka kwa kisingizio cha
kufuata familia zao na badala yake hawarudi tena na kufanya wilaya
hizo kuendelea kuwa na upungufu wa waalimu.
Akizungumza kwenye mkutano huo mkuu wa wilaya hiyo Agnes Hokororo
aliwataka wananchi na viongozi kushirikiana katika kuondoa changamoto
mbalimbali zinzosababisha maendeleo mabaya ya elimu wilayani humo.
“Iwapo viongozi tutashirikiana maendeleo ya elimu wilwywni kwetu
yatakuwa mazuri kwani suala la maendeleo ya elimu ni la kila mmoja
wetu”alisema Hokororo
Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa,Agness Hokororo(MB) Akiendesha kikao cha wadau wa Elimu wilayani Ruangwa Mkoani Lindi.
Baadhi ya Wadau wa Elimu wilayani Ruangwa Mkoani Lindi,wakifatilia kikao hicho.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...