Na Mwandishi Wetu
MAZOEZI kwa ajili ya kujiandaa na shindano la
kumsaka malkia wa Mkoa wa Tanga mwaka huu
"Redd's Miss Tanga 2013" yanatarajia kuanza Jumatano
Mei 8 kwenye Ukumbi wa Lavida uliopo jijini Tanga.
Akizungumza na Ripota wa Globu ya Jamii, Mkurugezi wa
Kampuni ya DATK Intertaimeint, Asha Kigundula ambae ndie Mratibu wa shindano hilo, alisema kuwa maandalizi ya
shindano hilo yanaendelea vizuri.
Kigundula alisema kuwa walimu watakaosimamia
warembo hao ni Miis Tanga 2012 Teresia Kimolo na
Miss Tanga 2011 Zubeda Seif.
Alisema kuwa maandalizi yanaendelea vizuri, ambapo
warembo wameanza kuitikia wito wa kushirikishi
shindano hilo.
Kigundula alisema kuwa mpaka sasa jumla ya
warembo 8 wamejitokeza kushiriki shindano hilo
ambapo nafasi bado iko wazi kwa wasichana wote
wenye sifa za kushiriki.
"Kila kitu kinaendelea vizuri, ikiwa na warembo
kuendelea kujiandikisha kushiriki shindano la mwaka
huu, ambalo nina hakika litakuwa la aina yake"alisema
Kigundula
Alisema kwamba shindano la mwaka huu litaandika
historia mpya ya urembo mkoani humo kwa kuwa
Kampuni DATK imejipanga, hivyo mashabiki wa
mashindano ya urembo wa jijini hapo kwa ujumla
wakae mkao wa kupata raha.
Pia alisema fomu zinapatika katika ofisi ya Mwananchi
iliyopo Bandari Tanga ghorofa ya Nne, Five Brathers
kwa Nassa Makau iliyopo jijini humo, kwa Dar es
Salaam zinapatikana katika ofisi za Jambo Leo zilizopo
Jengo la Hifadhi Hause Posta.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...