Wadau mbalimbali wa Serikali,Wafanyabiashara na wanahabari toka Mikoa
ya Lindi,Mtwara na Ruvuma wanakutana leo katika warsha ya mashirikiano
ya kibiashara kwa mikoa hiyo wanakutana leo ili kujenga na
kubadilishana mawazo kwa lengo la kujenga uelewano na Ushirikiano
ambao utasaidia kutekeleza Dira ya kibiashara kwa Ufanisi.
Majadiliano hayo ya ushirikiano yatachangia katika kusukuma mbele
utekelezaji wa Dira ya Tanzania ya Maendeleo 2025 pamoja na juhudi
mbalimbali kuendelea utekelezaji wa Dira hiyo hauendani na shabaha ya
kuiwezesha nchi ya kipato cha kati inayojivunia maendeleo makubwa na
maisha bora ya wananchi.
Katika warsha hii mada kuu ni kuhamasisha Teknolojia kwa mageuzi ya
kiuchumi na kijamii Tanzania itawasilishwa ikienda sambamba na mada
ndogondogo ikiwemo Umuhimu wa Ubunifu katika mageuzi ya kiuchumi na
kijamii,Mchango wa Tehama,Ubora wa Viwango katika wilaya,usalama wa
watu na mali zao ikiwa pamoja na majadiliano ya Vikundi mada ambazo
zitatolewa na UDSM,COSTECH,TCRA,TBS na Polisi Makao Makuu
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara,Kanali Joseph Simbakalia
akifungua Warsha ya Majadiliano ya Ushirikiano wa Kibiashara kwa
Manufaa ya Umma Kikanda kwa Wawakilishi toka Mikoa ya Lindi,Ruvuma na
Wenyeji Mtwara,Kulia ni Samson Chemponda,Kaimu Katibu Mtendaji wa
Baraza la Taifa la Biashara na kushoto ni Saidi Masudi
Nahunda,Mwenyekiti wa TCCIA-Mtwara.
Wadau mbalimbali wanaohudhuria kikao cha
mashirikiano ya kibiashara kutoka mikoa ya Lindi Mtwara na Ruvuma
kinachoendelea katika Ukumbi wa Makonde Beach Resort-Mtwara. Na Abdulaziz Video-Mtwara
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...