Children from New Life Home in Dar es Salaam enjoy a ride on
a toy train during a charity family bonanza organized by Women Footprints
Initiative which provided a rare opportunity for children from orphanage
centers in Dar es Salaam to play various games and music and have a chance to
mingle with family members. The lively event was held at Leaders Club in the
city.
Tatu Issa from New
Life Home orphanage center in Dar es Salaam get a ‘face lift’ during a charity
family bonanza organized by Women Footprints Initiative which provided a rare
opportunity for children from orphanage centers in Dar es Salaam to play
various games and music and have a chance to mingle with family members. The
lively event was held at Leaders Club in the city.
One of the children from New Life Home orphanage center in
Dar es Salaam engages in jumping castle during a charity family bonanza
organized by Women Footprints Initiative which provided a rare opportunity for
children from orphanage centers in Dar es Salaam to play various games and
music and have a chance to mingle with family members. The lively event was
held at Leaders Club in the city.
Women Footprints Initiative ( WOFI) Neema Msuya, address the
media at charity family bonanza that provided a rare opportunity for children
from orphanage centers in Dar es Salaam to play various games and music and
have a chance to mingle with family members. The lively event was held at
Leaders Club in the city.
Watoto yatima washiriki
tamasha la hisani la WoFI.
Dar
es Salaam Mei 4, 2013: Shirika la Women Footprints Initiative (WoFI),
leo limefanya tamasha la hisani la familia lijulikanalo kama Cheza
Time na kushirikisha watoto kutoka vituo vya kulelea watoto yatima
ambao wamecheza michezo mbalimbali na kupata fursa ya kujumuika na ndugu zao.
Tukio hilo la aina yake limefanyika katika viwanja vya Leaders Club.
Meneja
miradi wa WoFI Neema N. Msuya amesema kuwa pamoja na kutoa burudani za michezo,
tamasha hilo pia limetumika kupata fedha za kusaidia vituo hivyo vya watoto
yatima na kuendeleza miradi ya wanawake inayoendeshwa na shirika hilo kwa lengo
la kusaidia watoto na kuwawezesha kina mama kiuchumi..
Alisema
kuwa kusudi kubwa ya shirika la WoFI ni kuwawezesha watoto hao kupata mahitaji
yao ya msingi ikiwa ni pamoja na kuwapatia elimu na kuyataka makampuni,
mashirika na watu binafsi kujitokeza kusaidia ili kuwajengea watoto hao msingi
imara wa maisha yao ya baadaye.
“Tamasha
la hisani la familia tunalofanya hapa
leo linakusudiwa kuwa tukio la kila mwaka ambalo, mbali ya kuhamasisha wahisani
kuchangia mfuko wa shirika, litatumika kama chombo cha kuwaunganisha watoto na
ndugu na jamaa zao huku wakiburudika na vinywaji baridi, michezo mbalimbali
pamoja na kucheza muziki”, alisema.
Tamasha
la leo lililovuta hisia za watu mbalimbali lilishuhudia watoto wachangamfu
wakishiriki michezo ikiwa ni pamoja na mpira wa miguu, kuruka, kuogolea na
kukimbia ndani ya gunia. Watoto hao pia walipata fursa ya kuonyesha vipaji vyao
vya kuimba na kucheza muziki.
Shirika
la WoFI ambalo siyo la kibiashara vile vile huendesha kampeni ya kuwaelimisha
wasichana walioacha shule kwa sababu mbalimbali kuachana na tabia hatarishi na
kujishughulisha na biashara halali ili kujipatia kipato cha kuwasaidia katika
maisha yao. Kampeni hii inafahamika kama Binti Amka.
Kampeni
nyingine inayoendeshwa na shirika hili inajulikana kama Jitambue uwezo wako Sasa ambayo
inawahamasisha wasichana wa shule za sekondari kusoma kwa bidii na kushinda
vishawishi vilivyo mbele yao na hatimaye kutimiza ndoto za kuwa na maisha bora
hapo baadaye.
Asante sana dada Neema kwa Moyo huo wa kuwasaidia hawa watoto waweze kutimiza ndoto zao.Kama una internet naomba uwawekee huu wimbo wa Brenda Fassie-Ag Shame Lovey(a.k.a Mi -do-do-do-do-do-laa-doo-tiiii) uwaburudishe na kuwapa mazoezi.Wimbo ulirekodiwa kama miaka 25 hivi iliyopita lakini mzuri sana kwa Watoto.
ReplyDeletehttp://www.youtube.com/watch?v=ocmywGu5LY4
David V
Asante dada neema kwa kuwasaidia hawa watoto mungu atakulipa kwa wema wako lakin jamani kuwachora michoro ya kishetani spider sijui nini na nini tuiache jamani najua hamuwezi kunielewa nisemacho lakin taifa la kiafrica kitanzania nilapotea tusipoangalia kwa kizazi chetu kuwalea maadili mema hawa watoto wetu sio kukopi kila kitu kilichopo huko majuu tafadhalini ndugu zangu tuangaliye sana jambo hili
ReplyDelete