Waziri Mkuu Pinda akizungumza kwenye viwanja vya Nyerere Skwea,mara baada ya kupokea matembezi ya mshikamano yaliyowajumuisha wasanii wa muziki wa kizazi kipya/Filamu pamoja na wadau wengine wa sanaaa mbalimbali bila kuwasahau Clouds FM ambao ndio walioratibu shughuli nzima ya matembezi hayo yakiwa na lengo la kuiomba serikali iendelee kuzilinda fursa zilizopo na ikibidi kuziongeza katika wigo mpana ili kukwamua maisha ya wasanii na vijana walioko katika nyanja mbalimbali,kama vile haitoshi matembezi hayo yalikuwa na ujumbe uliolenga kupinga uharamia wa kazi za sanaa hapa nchini.Aidha Clouds FM pia walizindua msimu wao mpya uliopewa jina la MADE IN TANZANIA ndani yake kukiwa na kampeni kubwa ya TWENZETU katika harakati ya kuihamasisha jamii kujivunia vya kwao.
Home
Unlabelled
Waziri Mkuu pinda alipozungumza akiunga mkono harakati za kupambana na wizi wa kazi za sanaa mjini dodoma.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


Mie siku zote sielewi kilio hichi cha wana sanaa, sio bongo tu, kutaka serikali iwalindie mali yao. Ni kama mimi nikitaka serikali inilindie shamba langu. Nakubali kuwa wizi wa kazi zao si kitu kizuri, nisichoelewa ni kwa nini sisi sote tulipie ulinzi wa njia zao za kukusanya utajiri wao, na angalia hivi baina yao ni matajiri kweli.Serikali iweke kodi maalum ya wasanii hawa ili iunde kikosi maalum cha kuchunga mashamba yao, siyo kutumia mfuko wa wananchi.
ReplyDeleteWakatabahu
Mbona mie sijaelewa nini? kilicho nyuma ya mradi huu,maana naona kama ni wasanii kuibiwa kazi zao,sio kuwa
ReplyDeletevyombo na wausika wote kuwa wameshirikiana au kushirikishwa katika hili,naona baadhi ya wasanii wa kizazi kipya tu na Clouds media ndio wapo mbele,sasa BASATA wapo wapi? Wizara ya Habari,michezo na utamaduni ipo wapi haina mwakilishi?
Bendi za taarabu na muziki wa dansi hazionekani hapa! wachekeshaji nao wamesusia harakati hizi au?
Kweli vita hivi vitakua na ushindi?
au labda Ruge na timu yake wanataka kuwanyang'anya vijiti wenzao kwa kujifanya wao ndio wenye uchungu na sanaa,mbona kampeni hii imekuwa kama mchezo wa kuigiza