Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe akitia saini katika kitabu cha ufunguzi wa maonesho ya bidhaa na huduma za maji na usafi wa mazingira ambayo yanafanyika mlimani City, Dar es Salaam.
Waziri wa maji Profesa Jumanne Maghembe akiwa katika banda la Plasco Ltd katika maonesho ya bidhaa na huduma za maji na usafi wa mazingira.
Waziri wa Maji profesa Jumanne Maghembe amewataka wataalamu wa maji kutafuta suluhu ya tatizo la upotevu wa maji linalozikabili mamlaka nyingi za maji barani Afrika.
Akizungumza katika uzinduzi wa mkutano wa siku tano wa wataalamu wa maji barani Afrika unaofanyika jijjini Dar es salaam jana, Waziri Maghembe aliwataka wataalamu kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo kwa kuangalia njia zaidi ya moja.
Pamoja na hilo alisema mamlaka hizi zinakabiliwa na changamoto nyingi zikiwamo za uharibifu wa vyanzo vya maji hali, wizi na upotevu wa maji na mabadiliko ya tabia nchi yanayosababisha upungufu wa rasilimali hii.
Aidha, alisema pamoja na matatizo hayo mamlaka hizi zinajiendesha kwa hasara na kuwataka wataalamu kutafuta suluhisho la jinsi ya kujiendesha kwa faida ambako kutaziwezesha kuwekeza zaidi.
“Kuna haja ya kuhakikisha mamlaka hizi zinajiendesha kwa faida na si kama hali ilivyo sasa ambapo mamlaka hizi zinajiendesha kwa hasara na kutegemea ruzuku kutoka serikalini” Alisema Maghembe.
Akimkaribisha Waziri wa Maji kufungua mkutano huu, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wataalamu wa Maji Barani Afrika (AfWA) Silver Mugisha alisema mamlaka nyingi zimekuwa zikichukua suluhu za matatizo ya nchi nyingine bila kuangalia mazingira husika kiasi kwamba suluhu hizo hazi tatui matatizo ya mamlaka za Afrika.
Alisema wakati umefika wa kutafuta suluhu kwa mamlaka za Afrika kwa kuangalia mazingira ya Bara la Afrika ambayo kwa nchi nyingi za Afrika zinafanana.
“Tunahitaji kuja na suluhu zinazoendana na mazingira yetu na si kuchukua suluhu kutoka nchi za Magharibi ambazo hazitatui matatizo yetu” alisema Mugisha.
Mkutano huu unawashiriki kutoka nchi 21 za Afrika pamoja na Hispania na Ufaransa ambao umeandaliwa na Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es salaam (DAWASA) kwa kushirikiana na AfWA ukiwa na kauli mbiu ni “Kupunguza Maji yasiyolipowa: Njia gani ni sahihi.”
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...