Akagua ufukwe wa ziwa Nyansa katika mwambao wa ziwa hilo kwenye kijiji cha Lupingu, wilayani Ludewa, na kuwambia wananchi wasihofu na maneno Malawi kuhusu ziwa hilo, Serikali ipo imara kuwalinda usiku na mchana.
*Akagua na kuimarisha uhai wa Chama ngazi za chini kabisa za matawi na mashina. Ahudhuria vikao vya mashina na wajumbe wa nyumba kumi yaliyoko ndani ndani vijijini na kufanya mikutano ya hadhara iliyojaa shamra shamra, apokea wanachama wapya kibao
*Akagua hatua zinazoendelea katika upembuzi yakinifu wa mradi wa makaa ya mawe na chuma Liganga, aahidi wanannchi kushirikishwa kwa karibu mambo yakiiva.
UKAGUZI MWAMBAO WA ZIWA NYASA
KATIBU Mkuu wa CCM, Kanali mstaafu, Abdulrahman Kinana (wapili kulia) na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye (kulia) wakiwa kwenye ufukwe wa ziwa Nyasa, kwenye mwambao wa ziwa hilo katika Kijiji cha Lupingu, Kata ya Lupingu Wilaya ya Ludewa mkoa wa Njombe Mei 29, 2013, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya Chama na kusikiliza kero za wananchi katika mkoa huo. Wengine ni Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe na Mbunge wa Mwibala Kange Lugora.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...