Akagua ufukwe wa ziwa Nyansa katika mwambao wa ziwa hilo kwenye kijiji cha Lupingu, wilayani Ludewa, na kuwambia wananchi wasihofu na maneno Malawi kuhusu ziwa hilo, Serikali ipo imara kuwalinda usiku na mchana.
*Akagua na kuimarisha uhai wa Chama ngazi za chini kabisa za matawi na mashina. Ahudhuria vikao vya mashina na wajumbe wa nyumba kumi yaliyoko ndani ndani vijijini na kufanya mikutano ya hadhara iliyojaa shamra shamra, apokea wanachama wapya kibao
*Akagua hatua zinazoendelea katika upembuzi yakinifu wa mradi wa makaa ya mawe na chuma Liganga, aahidi wanannchi kushirikishwa kwa karibu mambo yakiiva.
UKAGUZI MWAMBAO WA ZIWA NYASA.
KATIBU Mkuu wa CCM, Kanali mstaafu, Abdulrahman Kinana (wapili kulia) na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye (kulia) wakiwa kwenye ufukwe wa ziwa Nyasa, kwenye mwambao wa ziwa hilo katika Kijiji cha Lupingu, Kata ya Lupingu Wilaya ya Ludewa mkoa wa Njombe, leo Mei 29, 2013, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya Chama na kusikiliza kero za wananchi katika mkoa huo. Wengine ni Mbunge wa Ludewa, Deo Philikunjombe na Mbunge wa Mwibala Kange Lugora.
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
Halafu huyu mama Raisi wa Malawi (Mkuuwa Wilaya ya Malawi) anadai eti Ziwa looote ni la kweke?
ReplyDeleteDuuu Ufukwe mzuri namna hii?
Ohhhh, aghhh hapana!!!
Mimi ninachotaka mnipe Bunduki na Sare za Jashi hata kama ni za Mgambo zitatosha pamoja na viatu vya Mabuti ili nikabiliane na Malawi tena bila mshahara wowote!
Mdau wa kwanza,
ReplyDeleteAmecheleweshwa sana huyu mana!
Ilitakiwa atumiwe Majeshi achapwe vilivyo labda ange ghairi madai yake baada ya Kichapo.
Mhe. Raisi Kikwete ndugu yetu, kwa nini Majeshi tunapeleka Kongo DRC wakati sisi nchi yetu inavamiwa wakidai Ziwa Nyasa?
Baadhi ya mambo hatuwezi kutegemea UN iamue!
ReplyDelete1.Hivi Wananchi wote wakazi wa ukanda wa ufukwe wa ziwa akiwemo Kada wa Chama Mhe. Komba tutawabeba vipi?
2.Maji watakunywa wapi, kama Ziwa looote litakuwa ni la Malawi?
3.Kitoweo cha Samaki watapata wapi?
4.Uchumi wa Kanda ya Ufukwe wa Ziwa Nyasa unalitegemea Ziwa, wataishi vipi wananchi wa Tanzania ktk ukanda wa ziwa Nyasa?
5.Ina maana wakiingia ktk Boti kusafiri kutoka Kijiji Kimoja Ufukweni kwenda Kijiji kingine (Ndani ya Tanzania) ni Lazima wawe na Pasipoti !,,,kwa sababu wakiwa ndani ya maji tayari wapo Malawi!!!
KWA SABABU HIZO HAPO JUU (5) SIONI KWA NINI TUSIMPIGE MAMA JOYCE BANDA NA MAJESHI YAKE?
Mhe. Nape Nnauye hiyo kofia yako (yenge rangi za Bendera ya Tanzania) mama Joyce Banda akiiona huku mpo ktk Ziwa Nyasa analodai yeye ataanguka kifafa!
ReplyDeleteJamani ni macho yangu yana zeeka au naona mweshimiwa Kinana amepungua kilo vizuri sana. safi sana mweshimiwa. Bado Nape sasa, kitambi lazima kishuke ni vyema kwa afya yako.
ReplyDeleteyani malawi wachukuwe ziwa lote alafu sisi tubakie na ufukwe tu yani maji tusiyaguse?
ReplyDeletehaki ya nani tena tutaumizana nipo tayari kujitolea kubeba mtutu kama enzi za mwalimu na kuingia mitamboni kumtoa nduli malawi
ufukwe mwananaaa nikirudi mwaka huu nitafika hapo nipate upepo mwanana wa ziwa na milima
kwanza nishashituka sasahivi hata hatugawani tena na malawi tunawageuzia kibao ziwa lote ni letu wakitaka kipigwe kitanuka vibaya mno.