Airtel Tanzania imeendelea kutimiza dhamira yao ya kuwapatia wateja wake unafuu zaidi kupitia huduma yake ya AIRTEL YATOSHA nchini ambapo sasa wateja watafurahia Vifurushi vya Airtel Yatosha kwa masaa 25 kwa siku,   hii itawawezesha watanzania kufurahia kupiga simu mtandao wowote kwa gharama nafuu kwa muda mrefu zaidi.

Akiongea wakati wa uzinduzi wa Airtel yatosha masaa 25 Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando alisema” kuanzia sasa, huduma ya Airtel yatosha kwa siku itakua kwa masaaa 25 kuanzia pale mteja anapojiunga na huduma, yaani masaa 24 ya kuongea na kama vile haitoshi Airtel yatosha inakuongezea saa jingine moja la ziada. Sasa wateja wa Airtel watafurahi kupiga simu kwa gharama nafuu na kwa muda zaidi kuliko ilivyokuwa awali”.

 “Hii ni ya kwanza na pekee kutoka Airtel, Airtel yatosha itaendelea kuwa suluhisho la mawasiliano ya huduma za simu kwa watuamiaji na wateja wa Airtel nchi nzima ”. aliongeza Mmbando

Airtel yatosha ni huduma iliyoanzishwa ili kuleta kuvunja mipaka kwa watanzania na kuwawezesha kuwasiliana ndani na nje ya mtandaa kwa gharama nafuu. Kujiunga na huduma hii  piga *149*99# na atapata majibu papo hapo achague unataka Yatosha WIKI au Yatosha SIKU au Tosha ya Mwenzi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 07, 2013

    Airtel nina la kuwa lalamikia.

    Mwezi wa tatu nilinunua Moderm ya internet( kama sikosei kulikuwa na promotion) cha ajabu ni kwamba mtandao siku zote upo chini sana na bahati mbaya mara tu baada ya kununua nilisafiri nje ya nchi.Kwa maana hiyo hata siwezi wasiliana vyema na familia yangu,je kuna tatizo gani?

    AMA NINYAMAZE TU NA KAULI MBIO YA "AIRTEL YATOSHA"

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 07, 2013

    Hiyo siku ya masaa 25 wataitoa wapi waongo hawa?

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 07, 2013

    SAA 25 JAMANI SI MASAAA!!S

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 07, 2013

    Hawa jamaa wa mobille phone companies wako desperate kwa kuwa wanajua zipo kampuni ambazo zimeshapata usajili tayari, na ambazo zitahusika na DATA tu, hivyo kuzipunguzia kwa kiasi kikubwa, faida walizokuwa wamezoea kupata kwa huduma zao DUNI sana za Internet. Aidha, wanaelewa kuwa, jinsi ambavyo makampuni zaidi yanazidi kisajiliwa au kupewa leseni na TCRA, ndivyo hivyo ambavyo faida zao zitakuwa zinapungua siku hadi siku. Mwisho, mkonga wa taifa ukikamilika, masuala ya mawasiliano yatakuwa nafuu sana. Inabidi wao (kina airtel, Voda, tiGO, Zantel, etc) waanze tu kushusha bei za huduma zao mapema.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...