JESHI LA KUJENGA TAIFA (JKT) LINAWATANGAZIA VIJANA WALIOMALIZA KIDATO CHA SITA 2013 NA KUCHAGULIWA KUJIUNGA NA JKT KATIKA MAKAMBI YARUVU PWANI, MGAMBO TANGA, MSANGE TABORA, BULOMBORA KIGOMA, MARAMBA TANGA, RWAMKOMA MARA, MLALE RUVUMA NA KANEMBWA KIGOMA KURIPOTI KATIKA MAKAMBI HAYO TAREHE 24 JUNI 2013 KAMA ILIVYOTANGAZWA AWALI.

VIJANA HAO WARIPOTI KATIKA MAKAMBI WALIYOPANGIWA KAMA ILIVYOONYESHA KATIKA TOVUTI YA JKT WWW.JKT.GO.TZ. ATAKAYERIPOTI KAMBI AMBAYO HAKUPANGIWA HATAPOKELEWA. VIJANA HAO WALIPOTI WAKIWA NA VYETI VYA LEAVING VYA KIDATO CHA NNE AU CHA SITA KWA UTHIBITISHO

INASISITIZWA KUWA KUJIUNGA NA JKT KWA MUJIBU WA SHERIA NI LAZIMA, ATAKAYESHINDWA KURIPOTI ATAKUWA AMEVUNJA SHERIA NA ATACHUKULIWA HATUA ZA KISHERIA

VIJANA WATUNZE TIKETI ZAO WALIZOTUMIA KWENDA KATIKA MAKAMBI YA JKT. NAULI ZAO ZITAREJESHWA NA JKT WATAKAPORIPOTI KAMBINI.

VIJANA WALIOCHAGULIWA KATIKA AWAMU YA PILI NI WALE WALIOFAURU KWA DIVISIONI, II NA BAADHI YA DIVISION III MCHEPUO WA SAYANSI.

VIJANA WA KIDATO CHA SITA 2013 AMBAO MAJINA YAO HAYAKUORODHESHWA KATIKA TOVUTI HIYO, WATAJIUNGA NA JKT AWAMU YA TATU MWEZI SEPTEMBA 2013.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 24, 2013

    Vizuri sana

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 24, 2013

    hii nchi kama isiingie kwenye matatizo ifanye nini? angalia hao vijana waliopasi fomu 6 hakuna uwiano wa kidini katika mgawanyo , sehemu kubwa ya wanafunzi ni wakirist , lazima wasilam wapige makelele , na hii sio bahati mbaya bali imepangwa iwe hivyo. Nchi yetu ina watu waina mbili kuu kidini , na katika hao bila shaka wasilam ni wengi ndio maana hata serikali ilikataa kuweka swali la kuuliza dini katika dodoso , ikiwa mambo haya hayakurekebiswa ndugu zangu hii dunia ya sasa ni ya uwazi , mtapoteza mamilioni kutafuta kamati , sijui vikao nk , havitosaidia , kwanza muweke uwiano kidini , kikabila kirangi , katika kila sekta , angalieni nchi za ulaya kama uingereza mtaona mfano ulio bora.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 24, 2013

    Wewe anonymous wa pili hapo juu sijui hata kwanini Michuxzi ameposti hiyo komenti yako, wewe unasisitiza UDINI na UKABILA bila hata aibu, wakati sisi tunakazana kufuta udini na ukabila nchi hii msije kuuana eti eti wewe unasisitiza udini na ukabila uwepo unaakili timamu wewe? sijui wewe unatoka nchi gani? Jamani mwelewesheni huyo kabla hajasababisha tuchinjane hapa.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 24, 2013

    We anony #2 unaonesha jinsi gani ulivyo mdini. Kama mnakazania kupeleka watoto madrasa kuliko kwenye elimu dunia unategemea nini. Unataka mtoto wako hata kama amepata zero abebwe tu kisa kutafuta uwiano?

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 24, 2013

    Huyo msemaji wa pili naona tumsaidie sana si kidogo.
    Kupasi mtihani hakuangalii dini. Zamani niaka ya 70 mwalimu Nyerere ndiye aliyeanza kushusha makabila yalioyonekana kusoma sana ili wawe sawa na wasiosoma. Matokeo yake yanaonekana sasa.Hizi vurugu za udini, ukabila n.k ni serikali kurithi fikra za mwalimu.

    Sasa basi, wale waliokidhi vigezo naamini ndio waliochaguliwa. Kama tutaanza kuzingatia uwiano badala ya vigezo, hapo nchi itakwisha tunaiona.

    Huyo msemaji wa pili anasema waislamu wameachwa. Mimi naona huyo hapo juu afanye kazi ya kuhamasisha lile tabaka lililoachwa nyuma, likazane ili kufikia vigezo. tusitegemee sana kufanyiwa upendeleo hata kama vigezo hakuna .Huu sio uzalendo.
    Lakini inabidi nitoe pole kama kuna baadhi ya watu wenye fikra hizi.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 24, 2013

    Hao waliochaguliwa kujiunga basi wasiteswe kupindukia kama zamani. Wafanyishwe kazi zinazoleta tija kwao na kwa taifa.

    Badhi ya maafande hupenda kuwatesa watoto hawa mpaka wengine kuuawa.

    hii hutokana na uchaguzi wa viongozi wasiostahili

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 24, 2013

    Huyo wa pili michuzi kapendelea. Hiyo comment haikupaswa kuingia humu.
    HUYO yuko nyuma sana. hata nimeshindwa nisemeje maana kama anaweza kuandika maneno hayo hata akisoma maoni hawezi kuelewa

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 24, 2013

    Kweli Tanzania kuna mambo. Wewe anony#2 unatuacha na maswali mengi. Hivi bado unafikilia mambo ya udini na ukabila miaka ya leo? Badala yakupambana na maisha hili kuleta maendeleo ya kila mtanzania? Unasema tuangalie kama ulaya wanavyo fanya. Hivi unajua Ufaransa wanaishije au unasema tu basi?
    Vijana komaeni na mafunzo hili muweze kuendeleza nchi yetu kizalendo zaidi.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 24, 2013

    annon wa pili tafuta KITU SAHIHI kinachowafanya wakristo wawe mbele, ukikipata kwa USAHIHI kabisa, kazania hicho ongeza na kajuhudi kaziada utakuwa mbele yao sana! sio kulalamika na kupandikiza chuki. Ni rahisi kumshinda mpinzani wako kama utajua mapema mbinu gani atatumia dhidi yako kwenye mpambano huo.


    BRAIN

    ReplyDelete
  10. Afircan AsiaJune 24, 2013

    kaaaazzzi kweli kweli, msemaji no 2 uko nyuma sana ndugu yangu, huko UK unakosema kuna usawa wa udini upi hasa? Tumeishi huko na hatukuona unachokisema inawezekana umedanganywa. Tafakari kama hautaenda shule hautafanya mitihani na pia hautafaulu hivyo hauwezi kuonekana humu, swala la waislamu kuwa wengi nchini zaidi sina uhakika yawezekana umefanya utafiti ndugu yangu ingawa pia utafiti wako sidhani kama utakuwa sahihi kwa asilimia 100, lakini hoja si udini hapa hoja ni kuhudhuria na kuzingatia hayo masomo ili uhitimu. Kaa mbali na udini hauwezi kukubeba utajibeba mtu mwenyewe kwa juhudu zako binafsi msisubiri mbeleko.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 24, 2013

    huyo anahitaji msaada wa kisaikolojia

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...