Watoto wakiwa na mishumaa wakiwa katika maandamano ya kuadhimisha miaka 100 ya KKKT leo katika usharika wa Chuo Kikuu cha Tumaini,Makumira, Usa River, Arusha 
 Mkuu wa KKKT Askofu Alex Gehaz Malasusa.akiongoza maandamano
 Maaskofu katika maandamano

Washarika na watu mbalimbali wamejumuika leo katika maadhimisho ya miaka hamsini tangu kuunganika kwa makanisa saba ya Kilutheri nchini na kuunda Kanisa moja la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT).

Kilele cha maadhimisho hayo yaliyoanza jana kimeadhimishwa katika Dayosisi ya Kaskazini, usharika wa Chuo Kikuu cha Tumaini (TUMA - Tumaini University of Makumira), Makumira, Usa River, Arusha yakiongozwa na Mkuu wa KKKT Askofu Alex Gehaz Malasusa.

Watu wapatao 5,000 wanatarajiwa kujumuila katika maadhimisho hayo.

Wanahabari wa Redio Sauti ya Injili, Moshi Tanzania wakiripoti moja kwa moja kutoka katika viwanja hivyo, wanasema hali ya amani na utulivu vimetawala hadi sasa.

KKKT inatokana na makanisa yaliyoanza kutekeleza utume wa kueneza Injili zaidi ya miaka 100 iliyopita nchini Tanzania. Mnamo tarehe 19 Jini 1963, makanisa yaliamua kiweka nbali tofauti zao na kuunganika na kuunda Sinodi na baadaye Dayosisi. Hadi Mei 26, mwaka huu, KKKT imefanikiwa kuwa na Dayosisi 22 na Misioni 20 zinazotoa huduma mbalimbali za kiroho kwa washarika wake na huduma za kijamii kwa wote kama vile mashule, vyuo vya mafunzo ya ufundi, Vyuo vya Elimu ya Juu, mabenki, mahoteli, mahospitali n.k.

Viongozi wakuu walioiongoza KKKT hadi sasa ni:

  1. Askofu Stefano Ruben Moshi (1963 - 1976)
  2. Askofu Dk Sebastian Kolowa (1976 - 1992)
  3. Askofu Samson Mushemba (1992 - 2007)
  4. Askofu Dk Alex Gehaz Malasusa ( 2007 hadi sasa)


Maaskofu Moshi na Kolowa ni marehemu. 
Askofu Mushemba ni mstaafu



.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...