Balozi wa Tanzania Ubelgiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala akisalimia Marafiki wa Asasi ya Mikumi Kids waliokutana kwa ajili ya kuchangia Mikumi Kids leo katika Mji wa Wilsele Ubelgiji. Mikumi Kids inaendesha kituo cha Watoto Yatima cha Mikumi Kids Tanzania. Balozi Kamala aliwashukuru kwa kuchangia Watoto Yatima na amewaomba waendelee kuwasaidia. Kushoto kwa Balozi Kamala ni Tausi Mpagama Mkurugenzi wa Mikumi Kids.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Ankal shikamoo. Naomba tafadhali unirushie hili ombi langu hewani. Ingawaje watu wataliponda lakini mwisho wa siku nitapata ufumbuzi. Mimi ni msichana wa kitanzania na nina miaka 26 sasa. Nipo Uingereza kimasomo kwani nachukua masters katika mji uliopo nje kidogo ya London.
    Shida yangu kubwa ni kwamba natafuta marafiki wa kitanzania waliopo hapa Uingereza maana kwa kweli ankali nchi za watu zinachosha sana especial pale ambapo hauna mtu wa kubadilishana naye mawazo. Kwamaana tokea nimefika hapa mwanzoni mwa mwaka huu mpaka leo sijawahi kusikia au kuongea kiswahili hata kidogo, na chuoni waafrika wengi ni kutoka West, South na Central Africa. Basi hapo ni tabu tupu..!
    Please Ankal naomba husiache kunirushia hewani hii post yangu. Napatikana katika email yangu swailaura@yahoo.co.uk Ahsante Ankal nashukuru sana na ninaamini nitapata marafiki wa kubadilishana nao mawazo. Napenda kukutakia weekend njema.
    Laura Swai,
    Uingereza

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 10, 2013

    Pole sana dada, mimi nipo london, nitakutumia email wiki hii nipatapo muda. Ila angalia waosha vinywa wengi sana hapa kwenye globu ya jamii.

    asante

    Mdau london




    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...