TAARIFA ILIYOTUFUKIA CHUMBA CHA HABARI CHA GLOBU YA JAMII,INAELEZA KUWA MSANII WA MUZIKI WA KIZAZI KIPYADA LANGA KILEO A.K.A LANGA AMEFARIKI DUNIA MUDA MFUPI ULIOPITA KATIKA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI ALIKOKUWA AMELAZWA.

LANGA AMBAYE INADAIWA KUWA ALIPATWA NA MALARIA KALI SANA HALI ILIYOPELEKEA KUKIMBIZWA HOSPITALI SIKU YA JANA.

TAARIFA KAMILI ITAKUJA BAADAE.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 21 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 13, 2013

    Duh poleni sana wafiwa. RIP. Jamani Muhimbili malaria inawashinda kutibu?

    ReplyDelete
    Replies
    1. AnonymousJune 13, 2013

      Anayetibu ni yule aliyetuumba yeye ndio mpangaji wa kila jambo langa ndio kifo chake kimeshaandikwa sasa unamlaumu nani

      Delete
  2. AnonymousJune 13, 2013

    Jaman, n nini hiki??
    Rest In Peace Langa

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 13, 2013

    R.I.P LANGA ila wewe mdau wa kwanza inaelekea unapenda sana lawama

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 13, 2013

    Ndo hospitali zetu hz jamani.RIP Langa

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 13, 2013

    R.I.P bro pembele yko nyuma yetu

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 13, 2013

    Inasikitisha sana, vijana wadogo, chipukizi na nyota wa nchi.

    RIP LANGA- MAHFOUDH- ORYX GAS

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 13, 2013

    siyo lawama ila inawezekana ni wrong diagnosis. RIP

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 13, 2013

    R.I.P langa

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 13, 2013

    Malaria kama haikuwahiwa mapema ni kifo. Michuzi hichi kichwa na habari "Msanii mwengine..." sio kizuri. Binadamu wote ni sawa na wataondoka duniani wakati wowote. Tujitayarishe vizuri kwa safari hiyo sote.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 13, 2013

    Sipendi lawama bali tuzingatie maisha ya watu. Sometimes uzembe nao unaingia. Mgonjwa kaja badala ya kumtibu haraka mtu anajizungusha. Mpime damu,muongezee maji mpe dawa ya kushusha homa na malaria. Hivyo vyote vikifanyika katika dakika 15 mgonjwa anapowasili maisha hukuolewa. Bila shaka mgonjwa alikuwa akitapika sana hivyo alihitaji drip. Huyo mgonjwa ukimpatia dawa ameze atatapika yote. Hivyo mdau mie sipendi lawama bali naongea ukweli mtupu. Na ukiiyachukulia haya masuala kama fundisho wagonjwa wengi wataokolewa.

    ReplyDelete
    Replies
    1. FUMO ISMAILJune 14, 2013

      Hakuna hospitari ye'te dunian hata iwe na madaktari bingwa kiasi gan,huwa na mortuary(chumba cha maiti). Hiyo ni kwa 7bu,M/MUNGU pekee ndio mwenye mipango yote. R.I.P LANGA.

      Delete
  11. AnonymousJune 13, 2013

    Unadhani malaria ni ugonjwa dhaifu au rahisi kutibika? Mara ngapi umesikia tukiambia watu flani wanapolazwa muhimbili kua wana malaria kali na wakapewa rufaa toka muhimbili kwenda aghakhani na baadae hupelekwa nje.hivi nikweli mnh hawawezi kutibu malaria au huwa kuna vitu vinafichwa? How common for an adult person to get severe malaria? Tafakari chukua hatua.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 13, 2013

    Unavyolaumu, je hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa Langa? kwamba kulikuwa na uzembe, na hakuhudumiwa katika dakika 15?

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 13, 2013

    Kweli kabisa tiba kwanza kujizungusha baadae..tatizo wanaweka pesa mbele badala ya uhai wa mtu, wenzentu nchi zilizoendelea wanajali afya ya mtu kwanza tena watahangaika sana kuokoa maisha ya mtu, vifo vya uzembe ni vichache sana na huwa wanachukuliwa hatua kali sana ikibainika mtu kafa kwa uzembe hivyo wahusika wanaogopa na kujali sana..ila tusilaumu safari ya Langa ilikuwa iwe leo imekuwa na ameondoka iliyobaki tuwafariji wafiwa ..R.I.P LANGA

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 13, 2013

    R I P langa. Kazi yake mora haina makosa...

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 14, 2013

    wewe ulisema anayetutibu ndo aliyetuumba. Hata maandiko yanasema, "jisahidieni wenyewe kwanza" Ukweli utabakia palepale hela kwanza, utu baadaye. Vitu vingine kwakweli huwa tunampa Mwenyezi Mungu mizigo.

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 14, 2013

    R I P Langa, tutakukumbuka daima.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 14, 2013

    Hilo fungu kwenye Biblia linalosema "jisaidieni wenyewe kwanza" linatoka katika kitabu gani cha Biblia...? Acheni kudanganya watu. Sote tu wapitaji tu katika hii dunia..tutalaumu weeee lakini eventually that is our way all of us. R.I.P Langa

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 14, 2013

    Uzembe huanza na sisi wenyewe kwa kuto chunguza afya zetu na kuzitunza ipasavyo. Tunakwenda au kupelekwa Hospitali tunapozidiwa na kutupia lawama madaktari. Kila mmoja wetu awa na tabia ya kujizuia maambukizi ya aina yeyote.
    Na ule unga unga unakinzana na tiba.

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 14, 2013

    Ni njia ya wote jamani...RIP Langa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...