Katibu wa NEC ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro, akimlaki Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Ukombozi wa Palestina (PLO), Tayaseer Khalid ambaye pia ni mjube wa Halmashauri Kuu ya Chama hicho, alipowasili asubuhi hii, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam kwa ajili ya ziara ya Kichama, hapa nchini. Pamoja naye ni Wajumbe wa NEC wa PLO, Jehad Zneed na Saleh Raafat.

Katibu wa NEC ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro, akiwa na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Ukombozi wa Palestina (PLO), Tayaseer Khalid ambaye pia ni mjube wa Halmashauri Kuu ya Chama hicho, alipowasili asubuhi hii, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julisu Nyerere, jijini Dar es Salaam kwa ajili ya ziara ya Kichama, hapa nchini. Pamoja naye ni Wajumbe wa NEC wa PLO, Jehad Zneed na Saleh Raafat (Kushoto). Wapili kulia ni Balozi wa Palestina hapa nchini Dk. Nasri Abujasir.
Katibu wa NEC ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro, akizingumza Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Ukombozi wa Palestina (PLO), Tayaseer Khalid ambaye pia ni mjube wa Halmashauri Kuu ya Chama hicho, kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam. Kiongozi huyo anatarajiwa kuwa na mazungumzo na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kuanzia saa 3.30 asubuhi hii, kwenye hoteli ya Protea Courtyard, jijini Dar es Salaam. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO
Hivi kweli huyo mmoja wa wageni toka Palestina (Mdada) ndiyo kavaa t-shirt imeandikwa ''KISS ME STUPID'' au macho yangu!?
ReplyDeleteHivi wana wachukuliaje chama cha CCM1? Wenyeji wao kwa ujumla!?
Ningekuwa mimi ni Asha Migiro sijui ningesema nimepata dharura rais kaniita hivyo nimwache dereva tu au lah!
Hiyo ze-fulanaz ya huyo mama kwenye huo msafara nimeipenda
ReplyDeletemaskini mama wa watu...kavaa T-shirt imeandikwa " Kiis me... Stupid"?...
ReplyDeleteSasa huyo huko nyuma alovaa T shirt yenye maneno Kiss Me Stupid aliingiajeVIP loune? Jamani asiogopwe mtu! Aaambiwe hapa kwetu huingii, basi.
ReplyDeleteWanawake woooooote Tanzania tungekuwa tunajiamini kama huyu mama hakika tungefika mbali sana, hata maendelea yange kuwa makubwa. Kwanza anafanya mazoezi sana kila siku siunaona mwili wake ulivyo fiti, na pia ana jiheshimu na kujiamini kiasi kikubwa sana. Wanawake tumuige jamani, tuige busara yake, hekima na ukakamavu wake.
ReplyDeleteMh MNEC wa Palestina Amevaa Tshirt inasomekaje? KISS ME 26......
ReplyDeleteNini tatizo??ili mradi amejisitiri hakuja uchi, nakumbuka enzi zile za miaka ya themanini na tisini ya mwanzo wabongo wengi tulikua tunavaa fulana zenye maneno makali pengine zaidi ya haya tuyaonayo kwa huyu mgeni wetu, lakini kwakua hutukujua na hatukua na njia mbadala ilitulazimu tujitukanishe mbele za watu.Hapa naongelea enzi zile za DABWADA AU KILAKA, nguo ikitoboka hakuna kutupa ni kubandika kilaka tu ngoma mdundo na ajabu zaidi ilikua rangi ya kilaka haiendani na rangi ya nguo asilia,utakuta kilaka rangi nyekundu na nguo asilia rangi nyeupe.
ReplyDeleteHiyo mbaya sana!
ReplyDelete