Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wake wa Marais wa Afrika wakati wa hafla ya ukaribisho iliyofanyika katika ukumbi wa UN Millenium Hotel huko New York nchini Marekani tarehe 11.6.2013. Mama Salma yupo nchini humo kwa ajili ya kupokea tuzo maalum ya Millenium Development Goals; Women Progress Award. Wengine katika picha ni Mama Constancia Mangue Nsue de Obiang, Mke wa Rais wa Equatorial Guinea, Mrs Nana-Fosue Randal, Mwanzilishi na Rais wa Voice of African Mother's Inc.akifuatiwa na Mrs Denise Nkurunziza Bucumi na Mwisho ni Madam Traore Mintou Doucoure, Mke wa Rais wa Mali.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mke wa Rais wa Mali Madam Traore Mintou Doucoure wakati wa hafla ya ukaribisho iliyofanyika huko New York tarehe 11.6.2013.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na Mwanzilishi na Rais wa Shirika la Voice of African Mother's Inc.la nchini Marekani Mrs Nana-Fosue Randal wakati wa tafrija ya kuwakaribisha wake wa Marais kutoka barani Afrika watakaotunukiwa tuzo ya Millenium Development Goals itakayotolewa tarehe 13.6,2013.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa pamoja na wake wa Marais wa Afrika wakati wa tafrija ya kuwakaribisha iliyofanyika katika ukumbi wa UN Milenium Hotel tarehe 11.6.2013. Wengine katika picha ni Mke wa Rais wa Mali Madam Traore Mintou Doucoure, Mke wa Rais wa Equatorial Guinea Madam Constancia Mangue Nsue de Obiang na wa mwisho ni Mwanzilishi na Rais wa Shirika la Voice of African Mother's Inc la nchini Marekani Mrs Nana-Fosue Randal.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiingia kwenye tafrija akiongozana na Mke wa Rais wa Equatorial Guinea Madam Constancia Mangue Nsue de Obiang.  PICHA NA JOHN LUKUWI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 12, 2013

    Mama mkuu wa Tz. vitenge ndio vinakupendeza zaidi.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 12, 2013

    Mama JK umetokaje?hakuna anaekuweza kati ya hao wamama,umependeza

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...