WANACHAMA wa chama cha mapinduzi Kata ya mipingo Kijiji cha Matapwa wilaya Lindi Jimbo la mchinga wakicheza kwa furaha baada kuwapokea wanachama zaidi ya 120 waliohama chama cha wananchi cuf na kujiunga na chama hicho tukio limesababisha tawi la chama cha wananchi kubaki na mwenyekiti na katibu wake.
Mwenyekiti wa ccm mkoa wa Lindi Alli Mtopa akimkabidhi kadi ya CCM miongoni mwa wanachama 120 wa kijiji cha Matapwa jimbo la mchinga hadija Saidi aliyehama chama cha wananchi cuf na kujiunga na chama hicho.
Mwenyekiti wa ccm mkoa wa Lindi Alli Mohamed Mtopa akimkabidhi kadi ya CCM Fatuma hamisi mkazi wa kijiji cha Matapwa jimbo la mchinga aliyeyehama chama cha wananchi cuf na kujiunga na chama hicho.

Na Abdulaziz video

WANACHAMA wa chama cha wananchi (Cuf ) tawi la Matapwa Jimbo la Mchinga wamekiama chama hicho na kuamia chama cha mapinduzi huku wakiliacha tawi ili likibaki na wanachama wawili akiwemo mwenyekiti na katibu yake.

Tukio hilo limetokea jana kwenye mkutano wa adhara uliitishwa na mbunge wa jimbo la mchinga saidi mtanda wakati alipokuwa kwenye ziara ya kutembelea miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika jimbo.

Akizungumza kabla ya kugawa kadi kwa wanachama zaidi ya 120 wa tawi hilo lililokuwa ngome ya cuf katika jimbo Hilo la Mchinga kiongozi mwandamizi wa chama cha mapinduzi taifa Tambwe Hiza aliwataka wananchi wa kata hiyo kuachana na siasa za kichochezi zinazo sababisha uvunjifu wa amani badala yake wafanye kazi za kujiletea maendeleo yao.

Tambwe alisema hakuna chama kinachotawala duniani ambacho kinagawa fedha kwa wananchi wake kwa ajili ya kuendesha maisha yao ya kila siku bali ilani, na sera mzuri kama za ccm ndizo zinawafanya wananchi wao kuwa na maendeleo ikiwemo upataji wa huduma muhimu za kijamii kama vile. Maji, elimu, miundombinu pamoja na huduma za Afya.

Aidha Tambwe aliwaomba wananachi wa jimbo hilo ambao hawajajiunga na chama hicho kujiunga haraka na kuachana vyama vyenye itikadi za kibaguzi, kidini na kueleza kuwa chama Ccm ndicho chama pekee nchini chenye sera mzuri na mwelekeo wa kuwaletea maendeleo wananchi yake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 27, 2013

    Kweli Wanachama ni Wanachama tu, kwani kila hakuna kura dhaifu. Lakini kwa nini mnapenda sana kwenda huko "rural interior" kuwawinda wazee wasiokuwa na uelewa Mnawapa mashati ya kijana na wanaona tayari wameshafanana na Kikwete na Kinana. Shameful

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 28, 2013

    Mwenyekiti kanzu CCM hapo mezani ni nini hicho mbona kimekaa kama msala. Kweli ukereketwa una ari zake.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 28, 2013

    Hahahahahahaha mdau wa kwanza umesema ukweli kwani hata ukiangalia tu utapata jibu la hayo mavuno yenyewe.Umasikini wetu na ugumu wa kunasuka katika makucha ya kijani unachangiwa na mambo mno.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 28, 2013

    Hawa kweli mchinga mchinga, wamewang'amuwa wazee wenye sera mgando.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...