WANACHAMA wa chama cha mapinduzi Kata ya mipingo
Kijiji cha Matapwa wilaya Lindi Jimbo la mchinga wakicheza kwa furaha
baada kuwapokea wanachama zaidi ya 120 waliohama chama cha wananchi
cuf na kujiunga na chama hicho tukio limesababisha tawi la chama cha
wananchi kubaki na mwenyekiti na katibu wake.
Mwenyekiti wa ccm mkoa wa Lindi Alli Mtopa
akimkabidhi kadi ya CCM miongoni mwa wanachama 120 wa kijiji cha
Matapwa jimbo la mchinga hadija Saidi aliyehama chama cha wananchi
cuf na kujiunga na chama hicho.
Mwenyekiti wa ccm mkoa wa Lindi Alli Mohamed Mtopa
akimkabidhi kadi ya CCM Fatuma hamisi mkazi wa kijiji cha Matapwa
jimbo la mchinga aliyeyehama chama cha wananchi cuf na kujiunga na
chama hicho.
Na Abdulaziz video
WANACHAMA wa chama cha wananchi (Cuf ) tawi la Matapwa Jimbo la
Mchinga wamekiama chama hicho na kuamia chama cha mapinduzi huku
wakiliacha tawi ili likibaki na wanachama wawili akiwemo mwenyekiti
na katibu yake.
Tukio hilo limetokea jana kwenye mkutano wa adhara uliitishwa na
mbunge wa jimbo la mchinga saidi mtanda wakati alipokuwa kwenye ziara
ya kutembelea miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika jimbo.
Akizungumza kabla ya kugawa kadi kwa wanachama zaidi ya 120 wa tawi
hilo lililokuwa ngome ya cuf katika jimbo Hilo la Mchinga kiongozi
mwandamizi wa chama cha mapinduzi taifa Tambwe Hiza aliwataka
wananchi wa kata hiyo kuachana na siasa za kichochezi zinazo
sababisha uvunjifu wa amani badala yake wafanye kazi za kujiletea
maendeleo yao.
Tambwe alisema hakuna chama kinachotawala duniani ambacho kinagawa
fedha kwa wananchi wake kwa ajili ya kuendesha maisha yao ya kila
siku bali ilani, na sera mzuri kama za ccm ndizo zinawafanya wananchi
wao kuwa na maendeleo ikiwemo upataji wa huduma muhimu za kijamii kama
vile. Maji, elimu, miundombinu pamoja na huduma za Afya.
Aidha Tambwe aliwaomba wananachi wa jimbo hilo ambao hawajajiunga na
chama hicho kujiunga haraka na kuachana vyama vyenye itikadi za
kibaguzi, kidini na kueleza kuwa chama Ccm ndicho chama pekee nchini
chenye sera mzuri na mwelekeo wa kuwaletea maendeleo wananchi yake.


Kweli Wanachama ni Wanachama tu, kwani kila hakuna kura dhaifu. Lakini kwa nini mnapenda sana kwenda huko "rural interior" kuwawinda wazee wasiokuwa na uelewa Mnawapa mashati ya kijana na wanaona tayari wameshafanana na Kikwete na Kinana. Shameful
ReplyDeleteMwenyekiti kanzu CCM hapo mezani ni nini hicho mbona kimekaa kama msala. Kweli ukereketwa una ari zake.
ReplyDeleteHahahahahahaha mdau wa kwanza umesema ukweli kwani hata ukiangalia tu utapata jibu la hayo mavuno yenyewe.Umasikini wetu na ugumu wa kunasuka katika makucha ya kijani unachangiwa na mambo mno.
ReplyDeleteHawa kweli mchinga mchinga, wamewang'amuwa wazee wenye sera mgando.
ReplyDelete