Daladala moja inayofanya Safari zake kati ya Gongolamboto - Masaki imetumbukia mtaroni mapema leo asubuhi maeneo ya Magomeni Mikumi jijini Dar es Salaam,baada ya kutaka kuovertake gari ndogo aina ya Noah hali iliyopelekea kupoteza muelekeo kwa daladala hilo na kuingia mtaroni
lakini kwa bahati nzuri hakuna aliyepoteza maisha na watu kadhaa walijeruhiwa.
Askari Polisi wakiangalia ajali hiyo wakati walipofika kuangalia.
Askari Polisi akichukua maelezo ya baadhi ya abiria walikuwepo kwenye Daladala hilo,ambao waliumia baada ya kuingia Mtaroni.
Break Down ikinyanyua Daladala hilo.Picha na Mdau Krantz Mwantepele.
Bange mbaya jamani! Sumatra mpo na mnaona wavuta bange wenu?
ReplyDeleteHiyo mitaro ifunikwe sasa. Yaani,watu kibao wanakufa na hiyo mishomo. Jamani, Mkitengeneza Barabara, mue mnaweka na bajeti ya kufunika mitaro. Watu wazitumie hizo njia ziwe za kutembelea, kama walivyo fanya kisutu. Yaani, mtu hata huwezi kukwepa ajali, cause utatumbukia kwenye Mtaro.
ReplyDeleteNakubaliana na wewe mdau. Wavuta bangi wengi ndo hao hao madereva mabarabarani! unakuta mtu yuko kwenye msikano wakati hata leseni hana.
ReplyDeleteDuh! hii 109 ndio itavuta hiyo daladala?
ReplyDelete