Bima inayofuata maadili ya ki-Islam inayojulikana kama (Takaful) ilifungua milango yake nchini Kenya na kupata mafanikio makubwa karibu miaka miwili sasa. Kwa kawaida shirika lolote la bima linatakiwa nalo lijinunulie bima kwa ajili ya kujilinda ktk wakati ambao italazimika kulipa fidia zaidi ya uwezo wake, ima kwa sababu ya majanga ya kitabia (natural disasters), moto, mafuriko au tukio lolote kubwa ambalo litawapata wateja kwa pamoja.
Kitendo cha shirika la bima kujinunulia bima kinajulikana kama Reinsurance. Kwa upande wa bima inayofuata maadili ya ki-Islam kitendo hicho kinajulikana kama (Retakaful).
Imeripotiwa kwamba The Kenya Reinsurance Corporation ina mpango wa kufungua kwa mara ya kwanza Retakaful nchini Kenya, na maeneo mbalimbali ambayo tayari kuna soko la biashara hiyo yakiwemo Afirca ya Magharibi na Mashariki ya Kati.
‘Kuna mabadiliko ktk biashara ya bima na tunataka kufaidika nayo kikamilifu’ alinukuliwa akisema Ndugu Jadia Mwarania ambae ni mkururgenzi wa moja ya mashirika ya bima nchini Kenya.
Kwa taarifa zaidi kuhusu bima inayofuata maadili ya ki-Islam na ile isiyofuata maadili ya kiislam tembelea http://ijuebankyakiislam.blogspot.com
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...