Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja akimvisha cheo cha Mkaguzi wa Magereza Mwanafunzi Na. 2623 S/SGT Clementina Nzunda kwa niaba ya wahitimu wanzake 51 ambapo wametunukiwa cheo hicho tangu leo tarehe 10 Juni, 2013. Sherehe hizo zimefanyika leo katika viwanja vya Chuo cha Udereva na Ufundi Kingolwira, Morogoro.
Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja akimvisha cheo cha Mkaguzi Msaidizi wa Magereza Mwanafunzi Na 2623 S/SGT Clementina Nzunda kwa niaba ya Wahitimu waliomaliza Mafunzo ya Uongozi Daraja la Pili katika Chuo cha Udereva na Ufundi Kingolwira, Morogoro.
Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja akisikiliza Risala ya wahitimu wa Mafunzo ya Uongozi daraja la Pili na Kozi ya Ukuu wa Kambi(RSM) hawapo pichani leo katika Chuo cha Udereva na Ufundi Kingolwira, Morogoro.
Wahitimu wa Kozi ya Uongozi daraja la pili Kozi Namba 1 ya Mwaka 2013 wakiwa katika mwendo wa pole wakijiandaa kutoa heshima mbele ya Mgeni rasmi Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja hayupo pichani. Sherehe hizo zimefanyika leo katika Chuo cha Udereva na Ufundi Kingolwira, Morogoro.
Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja (aliyeko katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wahitimu wa Kozi ya Uongozi daraja la pili na Kozi ya Ukuu wa Kambi(RSM) Mara tu baada ya kufunga Mafunzo hayo leo katika Chuo cha Udereva na Ufundi Kingolwira, Morogoro.
Inaonekana huu ni msimu wa kupandishana vyoe kwa hawa jamaa. Lakini Hongereni labda lipo la maana munalolifanya.
ReplyDelete