Na Abdulaziz Video,Lindi
Timu ya Karikoo Fc ya mjini lindi Ilishuka dimbani kumenyana na
timu ya Abajalo Fc ya mjini Dar es salaam Kipute hicho kilichopigwa
katika dimba la ILULU uwanja ambao una historia ya kutoiruhusu timu
ngeni kuondoka na ushindi.
Mpira ulianza kwa kasi kwa timu zote kushambuliana kwa kasi, kadri
muda ulivyokuwa ukisogea Abajalo Fc walionekana kuutawala mchezo huo
kwa kuweza kufika langoni mwa Kariakoo Fc mara nyingi lakini ngome ya
Kariakoo FC ilikuwa imara, hada mapumziko timu zilikwa bila kwa bila.
Kipindi cha pili kilianza kwa timu ya kariakoo kuliandama lango la
Abajalo na kuweza kupata penalt ambayo haikuzaa matunda baada ya
Nahodha wa Timu ya Kariakoo Anafy Jamvi kushindwa kuiwezesha timu yake
kuongoza kutokana na kupiga penalti hiyo kwa madaha na mpira kwenda
nje.
Dakika chache baada ya kukosekana kwa penalti hiyo Kariakoo iliongeza
kasi na kuliandama kwa mfululizo lango la Abajalo na Mchezaji Muhsin
ndiye aliwainua mashabiki mara baada ya kufunga goli maridadi kwa
kupokea mpira wa cross uliopigwa na salum abdalah naye kupiga kichwa
maridadi na kutinga wavuni goli ambalo Hadi mwisho wa mchezo matokeo
yalibakia KARIAKOO LINDI 1-0 ABAJALO FC.
(Agg 3-2.), Matokeo ambayo ambayo yameivusha timu ya Kariakoo na
kujijengea matumiani ya Kurudi Ligi kuu Ya Tanzania Bara
Katika mchezo wa kwanza uliofanyika mwishoni mwa wiki timu ya kariakoo
ilitoka sare ya mabao 2-2 mchezo uliochezwa jijini Dar es salaam na
kwa matokeo hayo kariakoo imefanikiwa kusonga mbele katika hatua ya 3,
ambapo itacheza na mshindi kati ya FRANCE RANGERS (Dar) au AFRICAN
SPORTS (Tanga)
Mtanange ukiendelea
Furaha ya ushindi
Nyomi la Mashabiki.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...