Wakati Dar es salaam unaambiwa nenda kashangae feri ambapo shilingi inazama ila meli inaelea, kwa upande wa jiji la Singapore ni tofauti kidoooogooo.... Hapo unaambiwa nenda Marina Bay kashangae meli iko juu ya vikwangua anga...Hii ni mojawapo ya hoteli za kitalii maarufu san
a jijini Singapore yenye bonge moja la Casino. Kiingilio kwa wageni ni bure... kwa wenyeji dola mia za Singapore...
a jijini Singapore yenye bonge moja la Casino. Kiingilio kwa wageni ni bure... kwa wenyeji dola mia za Singapore...
Kiingilio kwa Wageni ni bure?
ReplyDeleteHapo Singapore pamekuwa ni Tanga kwa Wanawake wa Kitanga?
Yalimkuta Karumanzila kutoka Kigoma alipo wasili Jijini Tanga!
Maana Mjini TA, a.k.a Tanga Mwambao Tanga kunani, unaambiwa waja leo waondoka leo, alipofika hakuulizwa Fedha mwanzoni akapewa huduma za kukata na shoka halafu yeye mwenyewe kulingana na Takrima aliyopewa na aibu aliyojisikia kama mwanaume ANAZAMA MFUKONI NA KUTOA AKIBA YAKE YOOOTE MWENYEWE AKAMKABIDHI JIMAMA!!!
Ankal kazi yako kusifia vya wenzetu tu.Hao waheshimiwa hivi ahawaoni aibu kwamba nchi kam bongo ina ila rasilimali lkn wanashindwa kufanya vitu vikubwa vya kueleweka?
ReplyDeleteHii inaonesha kwamba wabongo sote kuanzia raia mpaka viongozi wetu vichwani tuna tope badala ya ubongo.
Wanaweza kujenga hivyo kwa sababu hawapikii mkaa wa kuni!
ReplyDeletehapo jopo zima la viongozi wapo huko kutalii.mmefika japani na sasa singapore. mmeona kwa wenzetu kulivyo kuzuri.mkirudi nyumbani hakuna
ReplyDeletemnachofanya kurekebisha miji yetu na nchi yetu. sijui tuna laana gani sie wabongo walahi?
sasa hio safari mbona hamkwenda na Dr Ndugulile aone employment opportunities, investment opportunities na mapato yatakayokusanywa na local governments!!
ReplyDeletemnapeleka viongozi wa shirika la nyumba ili iweje,acheni upuuzi na hamuoni aibu kuwakaribisha viongozi wa nchi nyingine kutembelea bongo,yaani ni aibu kuanzia jk airport,mmezidi kuwaumiza wananchi kwa kutumia hela zao bila ya kujifunza kutokana na ziara hizi
ReplyDeleteAlafu hakuna ubaguzi wa rangi au wa wala mabeparis....wote wanya fanya kazi pamoja...wahindi, wachina, waafrika, waazungu nakadhalika...with one goal in mind....build the economy and the country and MAKE MONEY tu...TENGENEZA HELA!...bila matatizo au msubufu kutoka serakali na mawaziri wao...etc...money money money
ReplyDeletehuko hawajilimbikizii mimali utaifa kwanza ndo mana mnashangaa.. umeona mifoleni ya kufa mtu huko? we si unaona miundo mbinu ya huko? huko kwetu bora liende aibuuu kubwa hata watani wa jadi wako juu!
ReplyDeleteKaka unashangaa nini mbona na sisi tunayo MELI lile JENGO LA AIRTEL pale Morocco Dar? Huoni kama ni meli ile?
ReplyDeleteHalafu kama hiyo haitoshi pia tuna NDEGE AIRBUS lile JENGO LA "UWT" pale opozit na St Peters Ostabei? Ndege utaiona vivuri kama ukiliangalia kutokea barabara inayotoka Lidaz huku.
We vipi Michuzi wewe? Tusijiangushe bana!