Wakati Dar es salaam unaambiwa nenda kashangae feri ambapo shilingi inazama ila meli inaelea, kwa upande wa jiji la Singapore ni tofauti kidoooogooo.... Hapo unaambiwa nenda Marina Bay kashangae meli iko juu ya vikwangua anga...Hii ni mojawapo ya hoteli za kitalii maarufu san
a jijini Singapore yenye bonge moja la Casino. Kiingilio kwa wageni ni bure... kwa wenyeji dola mia za Singapore...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 06, 2013

    Kiingilio kwa Wageni ni bure?

    Hapo Singapore pamekuwa ni Tanga kwa Wanawake wa Kitanga?

    Yalimkuta Karumanzila kutoka Kigoma alipo wasili Jijini Tanga!

    Maana Mjini TA, a.k.a Tanga Mwambao Tanga kunani, unaambiwa waja leo waondoka leo, alipofika hakuulizwa Fedha mwanzoni akapewa huduma za kukata na shoka halafu yeye mwenyewe kulingana na Takrima aliyopewa na aibu aliyojisikia kama mwanaume ANAZAMA MFUKONI NA KUTOA AKIBA YAKE YOOOTE MWENYEWE AKAMKABIDHI JIMAMA!!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 06, 2013

    Ankal kazi yako kusifia vya wenzetu tu.Hao waheshimiwa hivi ahawaoni aibu kwamba nchi kam bongo ina ila rasilimali lkn wanashindwa kufanya vitu vikubwa vya kueleweka?
    Hii inaonesha kwamba wabongo sote kuanzia raia mpaka viongozi wetu vichwani tuna tope badala ya ubongo.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 06, 2013

    Wanaweza kujenga hivyo kwa sababu hawapikii mkaa wa kuni!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 06, 2013

    hapo jopo zima la viongozi wapo huko kutalii.mmefika japani na sasa singapore. mmeona kwa wenzetu kulivyo kuzuri.mkirudi nyumbani hakuna
    mnachofanya kurekebisha miji yetu na nchi yetu. sijui tuna laana gani sie wabongo walahi?

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 06, 2013

    sasa hio safari mbona hamkwenda na Dr Ndugulile aone employment opportunities, investment opportunities na mapato yatakayokusanywa na local governments!!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 07, 2013

    mnapeleka viongozi wa shirika la nyumba ili iweje,acheni upuuzi na hamuoni aibu kuwakaribisha viongozi wa nchi nyingine kutembelea bongo,yaani ni aibu kuanzia jk airport,mmezidi kuwaumiza wananchi kwa kutumia hela zao bila ya kujifunza kutokana na ziara hizi

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 07, 2013

    Alafu hakuna ubaguzi wa rangi au wa wala mabeparis....wote wanya fanya kazi pamoja...wahindi, wachina, waafrika, waazungu nakadhalika...with one goal in mind....build the economy and the country and MAKE MONEY tu...TENGENEZA HELA!...bila matatizo au msubufu kutoka serakali na mawaziri wao...etc...money money money

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 07, 2013

    huko hawajilimbikizii mimali utaifa kwanza ndo mana mnashangaa.. umeona mifoleni ya kufa mtu huko? we si unaona miundo mbinu ya huko? huko kwetu bora liende aibuuu kubwa hata watani wa jadi wako juu!

    ReplyDelete
  9. ZeroBrainJune 07, 2013

    Kaka unashangaa nini mbona na sisi tunayo MELI lile JENGO LA AIRTEL pale Morocco Dar? Huoni kama ni meli ile?

    Halafu kama hiyo haitoshi pia tuna NDEGE AIRBUS lile JENGO LA "UWT" pale opozit na St Peters Ostabei? Ndege utaiona vivuri kama ukiliangalia kutokea barabara inayotoka Lidaz huku.

    We vipi Michuzi wewe? Tusijiangushe bana!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...