Na Ripota
wetu Washington
Kijana Edward
J. Snowden (pichani), mfanyakazi wa zamani wa wakala wa Usalama wa Taifa wa Marekani (NSA) aliyevujisha nyaraka nyeti zinazohusu
mawasiliano ya watu yanayonaswa na wakala hiyo kwa vyombo vya habari
amefunguliwa mashitaka ya kuvunja sheria ya Ujasusi na kuiba mali ya serikali ili
kuvujisha taarifa nyeti kwa gazeti la Guardian na Washington Post, Idara ya
Sheria ya nchi hiyo imesema.
Kila kosa
katika hayo matatu aliyoshtakiwa nayo yanabeba adhabu ya kifungo cha miaka 10
jela, na habari zinasema huenda akaongezewa mashtaka. Zaidi ya shitaka la wizi,
mashtaka mengine mawili ni kufanya mawasiliano yanayohusu taarifa za ulinzi wa
taifa, na kuwasilisha kwa hiari yake taarifa nyeti za kiintelijensia kwa mtu
asiye na idhini kuzipata.
Mashtaka
hayo yalifunguliwa Juni 14, 2013 na waendesha mashtaka wa wilaya ya Mashariki
ya Virginia, ambako ndiko kesi nyingi za usalama wa Taifa za Marekani huendeshwa.
Maafisa wa Marekani wamesema tayari wamewaomba maafisa wa Hong Kong, ambako
Snowden anaaminika amejichimbia, kumtia mbaroni wakati maombi ya kumpeleka Marekani
yakiandaliwa.
Jaribio
la kumhamishia Snowden nchini Marekani
huenda likasababisha zogo refu la kisheria ambapo matokeo yake hayajulikani.
Makubaliano ya kidiplomasia kati ya Marekani na Hong Kong yanahusisha pia
kipengele cha kutomhamisha mtuhumiwa yeyote wa kisiasa toka nchi moja hadi
ingine, ambapo Snowden anaweza kudai kuwa kesi yake ni ya kisiasa.
Maswala
yote ya Hong Kong yanayohusu usalama wa Taifa hushughulikiwa na Serikali ya
China huko Beijing. Katibu wa zamani wa Usalama wa Hong Kong Bi Ip ambaye sasa
ni mbunge amesema leo kuwa hakuna jinsi bali kukubaliana na Marekani na hati ya
kukamatwa Snowden ikija polisi wao watamsaka na kumtia mbaroni.
Hata
hivyo, Bi Ip amesema kwamba Snowden anaweza uhamisho wake kwa kudai
alichokitenda ni kosa la kisiasa, ama anaweza kuomba hifadhi ya ukimbizi, na
kwamba kesi aina hiyo huchukua hata miaka 10 kukamilika.
Juma
lililopita mamia ya watu waliandamana kwenye mvua nje ya ubalozi mdogo wa
Marekani mjini Hong Kong wakiwataka maafisa wao wasitoe ushirikiano kwa ombi
lolote la kumhamisha Snowden.
Mashtaka
kama anayokabiliwa nayo Snowden ni ya saba chini ya utawala wa Rais Obama, wakati
utawala wa marais wote waliopita ni
mashtaka matatu tu yaliyofunguliwa dhidi ya ofisa wa serikalikuvujisha taarifa
nyeti kwa vyombo vya habari.
Snowden,
ambaye Ijumaa iliyopita alitimiza umri wa miaka 30, alikimbilia Hong Kong mwezi
uliopita, baada ya kuacha kazi yake ya kijasusi katika kituo cha Hawaii.
Ameshavujisha taarifa kibao nyeti sana kwa gazeti la The Guardian, ambalo
limekuwa likichapisha mfululizo wa makala kuhusu serikali za Marekani na
Uingereza kusikiliza mawasiliano ya watu kwenye mitandao na simu.
Kwa kuvujisha
taarifa hizo nyeti, Snowden amefungua dirisha lisilotarajiwa kuhusu mwenendo wa
kiintelijensia wa N.S.A, ikiwa ni pamoja na kukusanya kwake kwa taarifa karibu
zote za simu zinazopigwa Marekani pamoja na mkusanyiko wa email za kutoka watu wan
je ya nchi hiyo kutioka katika makampuni makubwa ya mtandao, ikiwa ni pamoja na
Google, Yahoo, Microsoft, Apple na Skype.
Snowden,
ambaye alisema alishangazwa kwa kile alichoamini kuwa ni hatua ya NSA
inayoingilia mambo binafsi ya Wamarekani na watu wan je ya nchi hiyo,
aliliambia gazeti la The Guardian kwamba amevujisha nyaraka hizo nyeti kwa kuwa
anaamini mipaka ya kufuatilia habari za watu iamuliwe sio na maafisa wa
serikali bali rais wa Marekani.
Mambo kama hayo yanaweza tokea hata huku kwetu. Hivyo idara za usalama inabidi kujifunza na kutobadilisha mifumo ya kuwapata vijana waadilifu na wazalendo wa kweli kufanya kazi nao.
ReplyDeleteSasa kijana hakuweza maliza masomo yake, pia hata kwenye mafunzo ya kijeshi hakuweza kufuzu vizuri yote hayo ni viashilia vya kuwa na mashaka. Hila jamaa wakakomaa nae wakampatia kazi.
Soma kwa idara zetu pia, vetting izingatiwe sana.
Mzuri Huyo natamani awe mume wangu .
ReplyDeleteWho care!
ReplyDeletei agree with snowden bcoz of free speech and that of unright of communications freedom.
ReplyDelete