CAPTAIN JUMA KASEJA NA KIKOSI CHAKO CHA KAZI, NAPENDA KUWATAKIA KILA LA KHERI KESHO MTAKAPOTINGA HAPO VIWANJA VYA GRAND STADE MJI WA MARRAKECH KUPAMBANA NA MOROCCO.
NINA IMANI YA KUWA WATANZANIA WOTE TUKO NYUMA YENU, TUNAWAAMINI NA TUNATHAMINI UZALENDO WENU. TUNA IMANI YA KUWA MTATUMIA WEMBE ULEULE MLIOWANYOLEA HAWA WAMOROCCO UWANJA WA TAIFA NA KUWABWAGA 3-1, KWA MAKALI YALE, AMA ZAIDI KWA NIA MOJA TUU YA KUFIKA BRAZIL 2014 ……
PAMOJA NA SALAMU NAPENDA KUWATAARIFU KUWA WANA DIASPORA WA LONDON TUMEJIPANGA VIZURI ILI KUWA NYUMA YENU KATIKA SAFARI YOTE . KIKOSI KABAMBE CHA WASHANGILIAJI, KIMEONDOKA LONDON JIONI HII KUJA MARRAKECH ILI KUWAUNGA MKONO.
KIKOSI HICHO, KIKIONGOZWA NA “MEYA WA JIJI”   SIR.HARUNA MBEYU, KITAKUWA PALE “GRAND STADE” NA MAVUVUZELA YA HATAREEEE TAYARI KWA MPAMBANO HUO. 
TUKO BEGA KWA BEGA NA NYINYI MPAKA 2014 NDANI YA “ESTADIO DO MARACANA”, RIO DE JANEIRO……
NAWATAKIA USHINDI MKUBWA NA MCHEZO MWEMA “FAIR PLAY”.
MWENYEZI MUNGU IBARIKI TAIFA STARS.
MWENYEZI MUNGU IBARIKI TANZANIA.
TAIFA STARS OYEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE……………!!
Mariam Mungula -MwanaDiaspora

#TeamTaifaStarsUK.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 08, 2013

    Asanteni sana wanadiaspora wa UK kwa uamuzi wa kwenda Morocco kuishangilia Stars. Hii ni motisha ya kutosha kuisaidia timu yetu. Inshallah tutashinda! - Kilakshari

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 08, 2013

    Mechi inaonyeshwa channel gani jamani

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...