Tanzania kama nchi nyingine zinazoendelea na zinazotegemea kilimo, imetoa mtazamo wake wa jinsi suala la kilimo linavyotakiwa kushughulikiwa katika ngazi ya kimataifa hasa pale suala hili litakavyohusishwa na mabadiliko ya tabianchi.
Hayo yamewasilishwa leo na Bi Emelda Adam, afisa mazingira mwandamizi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais katika mkutano unaoendelea hapa mjini Bonn, unaojadili pamoja na mambo mengine jinsi gani sekta ya kilimo itakavyoweza kuhimili athari za mabadiliko ya tabianchi na pia itakavyochangia kupunguza gesi joto.
Akiwasilisha msimamo wa Tanzania, Bi Emelda asema kuwa sekta ya kilimo ni mojawapo ya sekta muhimu katika uchumi wa nchi nyigi za Afrika . Aidha sekta ambayo inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo kuaathirika sana na mabadiliko ya tabianchi kutokana na sekta hii kutegeme sana hali ya hewa.
Hivyo amesisitiza kuwa kipaumbele kiwekwe katika kuangalia ni jinsi gani nchi hizi zitaweza kuongeza uzalishaji ili kuhakikisha usalama na upatikanaji wa chakula bi Emelda ameendelea kusema kuwa, kuna haja ya kuhakikisha kuwa kipaumbele kinakuwa katika suala zima la kuhimili mabadiliko ya tabianchi.
Tanzania ikiwemo katika kundi la nchi maskini dunini, imesisitiza kuwa suala la upunuzaji wa gesi joto liangaliwe katika muktadha wa maendeleo endelevu , kwa mtazamo kuwa iwapo mifumo bora itawekwa ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa nchi hizi zinawezeshwa katika matumizi ya teknologia za kisasa katika suala zima la uzalishaji wa chakula, kunaweza kusaidia kuongeza uzalishaji wa chakula na wakati huhuo kupunguza gesi joto zitokanazo na sekta hiyo.
Aidha, Imeongezwa kuwa Utafiti na Teknolija zitakazo saidia kujenga uwezo wan chi zinazoendelea kuhimili mabadiliko ya tabianchi ni suala linalotakiwa pia kupewa kipaumbele katika majadiliano hayo.
Mkutano huu wa mabadiliko ya tabia nchi ni moja ya mikutano ya utangulizi kuelekea mkutano mkubwa wa dunia wa 19 wa nchi wanachama wa mkataba huo, utakaofanyika Warsaw nchini Poland mwezi December.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...