
Bendi hiyo imefanikiwa kutwaa tuzo hizo mwishoni mwa wiki
iliyopita ambapo utoaji wa tuzo hizo ulifanyika Mliman City Dar
es Salaam.
Akizungumza jana Dar es Salaam, Meneja wa bendi hiyo Martin
Sospeter, alisema kuwa ni jambo la kumshukuru Mungu na kila
mdau wa muziki kwa kuweza kutupigia kura na kupata tuzo
hizo.
Alisema kuwa kwa namna moja au nyingine bila ya kupata
ushirikiano wao wasingeweza kufika hapo.
Alisema kuwa kupata kwao kura nyingi zilizoiwezesha bendi yao
kufika hapo ni kutokana na kupata ushikiriano mzuri toka kwa
vyombo vya habari.
Sospeter alisema kuwa hivyo wamejipanga kuhakikisha
wanafanya vizuri katika albam yao ijayo, ambayo utambulisho
wa nyimbo tatu utafanyika mara baada ya kumalizika kwa
mwezi mtufu wa ramadhani.
"Tunashukuru sana kwa kutupa ushirikiano mzuri kwa kuweza
kupata kura nyingi zilizoweza kutupa tuzo tano,"alisema
Sospeter.

Rais wa bendi hiyo,Charles Gabriel maarufu kwa jina la Chalz
Baba alisema kuwa tuzo hizo yeye pamoja na bendi yake
wamepata nguvu mpya ya kufanya kazi zaidi na kujituma na
kuahidi kuwa albamu yao mpya itakuwa kali ikiwa na lengo la
kutoa shukrani ya kukubalika kwao kwa Watanzania.
"Nitumie nafasi hii kutoa pongezi kwa kila mmoja, ni vigumu
kukutana na watu wote kuwashukuru lakini kwa kutumia fursa
hii naamini wengi watafahamu namna ambavyo tunatambua
mchango wao wa sisi kufika hapa.Usiku wa Kill Music Award
mwaka huu umeandika historia kubwa katika bendi
yetu,"alisema.
Rapa maarufu wa bendi hiyo, John Saulo a.k.a Furgeson,
alisema kuwa ni furaha kwake na familia ya mashujaa bendi,
kwa kuweza kuthibisha kile wanachokifanya, hivyo anapenda
kutoa shukrani kwa wote waliosababisha wafike hapo.
Aliongeza kuwa anatambua namna bendi yao ambavyo
inakubalika hata pale ambapo wanafanya onesho sehemu lakini
kitendo cha mashabiki, wapenzi na v yombo vya habari katika
jitihada zao imesaidia wapewe tuzo hizo.
"Tuzo hizi zimefungua ukurasa mpya kwetu, lakini pia
imepunguza maswali kwa baadhi ya wale ambao waliokuwa
wanatubeza na kutuona kama hatuna
tunachokifanya,"alisisitiza.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...