Kaka Michuzi naomba kuweka hili tangazo ili sisi wahanga wa Meli ya C Ladybug iliyokamatwa Antwerp Port kutokana na matatizo ya mwenye meli kama ujuavyo hii meli ni kubwa sana na ilikuwa na vitu vinavyokuja Tanzania vyenye thamani zaidi ya Dollar million tatu, kitu ambacho kimetusababishia matatizo makubwa sana kutokana na mipango yetu kuvurugika, kwa hadi sasa kuna kila dalili za kutumia pesa nyingine ili ku faulisha mzigo na kupakia kwenye meli nyingine kuja Tanzania. 

Katika hali ya kawaida sisi haituhusu kwani tumelipa gharama shipping hadi Dar es salaam Port na Sio Antwertp. Ukweli ni kwamba TMT Group ambao ni wenye meli ndio wenye matatizo  sisi tunadeal na RORO Line ambaye ni operator wa hizi ambaye bado anauwezo wa kututafutia meli nyingine kuendeliea na safari lakini hatoi ushirikiano katika kutatua tatizo hili.

Kama kuna mtu yeyote mwenye mzigo kwenye meli naomba tuwasiliane ili kuongeza nguvu kwenye hili suala, hizi ni contact zangu kwa maelezo zaidi.
Tel: +44 7410 792266

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 06, 2013

    Mbona hueleweki vizuri, tatizo ni nini hasa? Mwenye meli unasema ana tatizo mbona husemi wazi ni lipi? Kibongobongo! Akili ni nywele mana hapo kama kuna utapeli mnalwo. Wenye mizigo wamelipia wawasaidie nini? jamani mambo mengine yanaweza kumpa BP mwenye mizigo ukizingatia thamani ya vitu vilivyomo humo. Mhusika arekebishe tatizo na sio wateja wenu.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 06, 2013

    mdau pitia mtandao huu utapata ripoti za kusaidia kidogo

    https://www.facebook.com/SchivoCars/posts/444651178945973

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...