Alvin Walter Makundi ni kijana mdogo wa Kitanzania anayeishi na wazazi wake nchini Singapore. Akiwa na umri wa miaka 14 na mwanafunzi wa kidato  cha pili  huko Singapore, tayari ameshatumbukiza jina lake katika orodha ya wataalamu wa application katika moja ya makampuni makubwa duniani ya kutengeneza simu za mkononi ya NOKIA, ambapo anatengeneza applications ambazo  anazituma katika kampuni hiyo ambayo nayo bila hiana huitumia. Kwa idhini ya mama yake Globu ya Jamii ilipata fursa ya kuongea naye kuhusu hayo maajabu anayoyafanya. Msikilize. hapo chini...

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Bw. Walter P. Makundi, ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania waishio Singapore siku alipokutana na kuzungumza nao. Bw. Makundi, ambaye ni Meneja mradi wa kampuni kubwa ya ujenzi ya APCO PTE LTD ya hapo Singapore, ndiye baba mzazi wa Alvin. Kulia kwake ni mkewe, Mama Alvin.
Chini Rais Kikwete akisalimiana na Alvin ambaye aliongozana na mama yake pamoja na dada kuja kumuaga wakati Rais akiondoka Singapore usiku huu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 06, 2013

    Super proud of you Alvin.....!!!!!
    Keep it up... !!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 07, 2013

    Big up boi.

    Ankali piga kazi .zee hiyo post yako unaweza kuja kuwa rais wa bongo huko mbeleni kwani hakuna kisichowezekana

    Angalia mkapa yule pale alitokea hukohuko kwenye habari na uhandishi
    Wabongo hatuna makuu mtu wowote anaweza kuwa rais wetu muhimu asiwe na upungufu wa akili tu.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 07, 2013

    wewe anony wa pili acha kejeli zako. ASANTE MICHUZI KWA KUWEZA MAWAZO YAKE ILI KUMFANIKISHA HAJA YAKE.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 07, 2013

    wewe anon unaemsema mwenzio wa pili kuwa ana kejeli alichokosea ni nini ? kwani haiwezekani ankali akawa mgombea wa urais? au wewe ndio wale wenye imani za kuburuzwa kila siku kwani ankali sio mtanzania mwenye sifa za kuwa kiongozi?
    mwache mwenzako ana haki ya kutoa maoni wacha matusi

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 07, 2013

    Huyo Dogo ni MKALI sana. Wamtoe huko Singapore akasome MIT. Serekali inatakiwa fadhili watoto kama hawa maana future Jamani mambo yatakuwa ni E-everything. Hata vita zitakuwa sio tena kupigana makombora, kutakuwa na E-wars etc. So tukiwa na Wanajeshi wetu kama hawa mapemaa ndio watakuwa majenerali. wish ningepata contact za huyu dogo. Am so HAPPY. Alafu Dogo anaonekana anapenda OPEN SOURCE, as anasema hataki hela mbele. very good. Ila utapata hela sana huko mbele,continue na open spource kwa sasa as unakaa kwa wazazi ila baadae think of making Money.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 07, 2013

    Thank ankal michuz kwa hii post. By then mi nitampataje huyu kijana coz you didn't put his contacts. I really want to learn from him for my upcoming FYP in apps. that i'm currently focusing to do. I live in malaysia not far from singapore and my email:issaramadhan87@yahoo.com
    i will appreciate ankal if u'll manage to do that.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 07, 2013

    SI kwamba watoto wetu wanafeli kwa kuwa hawana akili...wangesoma kwenye mazingiraa mazuri ya kielimu tungekuwa na kina Alvin wengi,; hata Alvin angekuwa huku wala asingefika hapo alipo....TAFAKARIiiii

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 07, 2013

    Patrick, huyu mtoto anaonekana anajua kiswahili ila Ankal ndiye aliyeanza kumhoji kwa kiingereza. Ila pia Ankal ni bonge la marketer manake, amempa PROMO la nguvu. watu wa makampuni mbali mbali wanaweza kumsponsor ili awe programmer au app developer wao. sasa wewe unayetaka kila mtu aongee kiswahili ni ili kukurahisishia uelewa au? Tuweni na business strategies kwenye kila nafasi tunazopata kutokea kwenye TV unless unahojiwa kuhusu mambo ya kifamilia kama harusi/msiba. Huu sio wakati wa kuongea kiswahili eti kisa wewe ni mtanzania.

    Nakupa mfano mmoja wa yule dada mchekeshaji wa Uganda, Anne Kansiime, nenda you tube uangalie clips zake,huwa anatoa za kiingereza na nyingine kwa kiganda. chungulia anazotumia kiganda,watu wanatoa comments gani? sasa wewe kama umekalia uzalendo wa lugha wakati wenzio wako kibiashara zaidi,itakula kwako..

    otherwise, Big up Alvin..Do your thing and May God Bless you.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 07, 2013

    michuzi usibanie sema mtoto wa KICHAGGA. huku nyumbani hamtupendi na mnajaribu kutuzibia riziki zetu. bahati nzuri WACHAGA tunatesa tu hata nje ya nchi.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 07, 2013

    makundi ni wachaga? we mdau hapo juu acha ukabila, huyo ni mtoto wa kitanzania, tuache udini na ukabila, matatizo tuliyonayo yanatutosha

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 07, 2013

    yes toto la kichagaa wachaga ndo wenyewe akili kwenda mbele mungu ambariki sana na watu wasimtiye mdomoni na vijicho vyao vya nuksi sometimes its a good thing unajitoa kwenye blog but sometimes its a good thing unafanya vitu vyako chini kwa chini ukija ibuka watu wanakushanga tuu lakini hawajui plan zako

    unafikiri hao wazungu au mtu yeyote atakaye mpa support ontop of the sky atakuwa kwa nia njema au kutengeneza pesa

    dogo fanya hizi apps zako ziwe una zio own mwenyewe na fanya kwa pesa bwana dunia pesa na biashara

    wachaga akili kwenda mbele big up dogo

    na wazazi wadogo nakupeni hongereni sana tena mumuangalia sana mtoto wenu kuna mafisi wantaka kumnyakua kwa kipaji chake hiki mchunge sana na mafisi na simba hawa wenye kutaka mteremko

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 08, 2013

    mbona yule mbongo alie tengeneza facebook ya bongo www.mvuto.com hamkumsapoti?? Jamaa alijitahidi kuwaunganisha wabongo wote ulimwenguni lakini wachache ndio wamemsapoti. Mimi binafsi nilipendezwa sana na kazi aliyoifanya kama final thesis yake. Michuzi naomba umuunganishe huyu dogo na jamaa wa mvuto.com kwakeli niwatanzania wanaojitahidi. Pig up sana dogo!!!

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 08, 2013

    HUYO MTOTO NI MALI YA 'JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA'

    TENA JAMBO ZURI NI KUWA KULINGANA NA KAULI ZAKE INAONYESHA HUYO MTOTO NI MWANANCHI MZURI NA MZALENDO SANA KWA KUPENDA UWAZI NA KUTOTAKA FEDHA MBELE NI WAZI ATAKUWA SIO KIZAZI CHA KIFISADI NA UBINAFSI WALA UKABILA,,,MUNGU ATAMZIDISHIA NA KUJA KUITUMIKIA VYEMA NCHI YETU INAYO KWENDA MRAMA!

    Kwa sababu HAKUNA TAIFA LA UCHAGGA hata baba yake analifahamu hilo!!!

    ReplyDelete
  14. da jaman twende mbele turudi nyuma hakuna taifa la wachagga lakini hili kabila limejaliwa so tungekuwa tunatoa elimu nzuri tupo wengi sema ndo hivyo wengine tunawajua ila ndo hivyo tena yaani roho inaniuma tatizo ni hili ndugu zangu huku mashuleni vyuoni hatufundishi kuelewa tunakalilishwa jamani theories nyingi kuliko real practicals unadhani hao kina ALVIN tutawapata wapi ila wapo wanaojitutumua wanaonekana hawana kitu ndo hivyo tena tubadilishe real practicals ziwe nyingi tupunguze theories ila HAKUNA MJINGA TZ

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...