Wajuzi wa mambo wanasema kisa cha kupopolewa kwa chupa wakati akiburudisha huko Dodoma usiku wa jana, ni kutokana na taarifa zilizoandikwa kwenye gazeti moja la udaku kuwa alimsema vibaya mwanamuziki mwenziye ambaye sasa ni marehemu, aliyefia nje ya nchi, kuwa aliaga dunia akiwa masikini na kutumia dawa za kulevya kutokana na msongo wa maisha yaliyomwendea kombo.
Ingawaje mwenyewe alisema amenukuliwa vibaya na magazeti hayo yanalenga kuuza kwa habari za uzuri, aliomba samahani kwenye ukurasa wake wa Facebook na kuahidi kwenda nyumbani kwa wazazi wa marehemu kuwataka radhi.
Lakini inaelekea jitihada zake hazikufanikiwa kiasi cha kupatwa na zahma asiyoitarajia usiku wa jana.
Ikiwa ndivyo yaliyo, inaonesha ni kwa kiasi gani wananchi wanaamini na kutilia maanani vinavyoandikwa na kutangazwa kwenye vyombo vya habari.
Laiti nguvu ii hii ya kuyapa kipaumbele masuala ya burudani ingewekwa katika kuyasaka maarifa thabiti ya elimu na kujiendeleza, pengine kila kaya na nchi ingekuwa iko katika hatua kubwa ya kimaendeleo.
Source: http://www.wavuti.com/


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...