Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Billal akisoma moja ya vitabu vya uhifadhi wa mazingira wakati akikagua banda la maonyesho la Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira kwenye kilele cha siku ya mazingira kitaifa Mkoani Rukwa katika Mji mdogo wa Namanyere wilayani Nkasi leo tarehe 05.06.2013, Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt. Rajab Mtumwa Rutengwe. Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira Dkt. Terezya Luoga Huvisa.

Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Billal akipanda mti wa kumbukumbu katika kampeni ya uhifadhi wa mazingira mbele ya Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi leo tarehe 05.06.2013 ikiwa ni kuadhimisha siku ya mazingira duniani ambayo kitaifa imefanyika Mkoani Rukwa.
Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Billal akizindua kwa kuwasha mashine mpya ya maji katika bwawa la maji Mphiri ambalo ni chanzo kikuu cha Maji katika Mji mdogo wa Namanyere Wilayani Nkasi leo tarehe 05.06.2013. Serikali imetenga jumla ya Tshs bilioni nne (4) kuendeleza chanzo hicho muhimu ambacho asili yake ni chemchem.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI




Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...