Na Anna Nkinda 
Watumiaji wa lugha ya Kiswahili wamezidi kuongezeka nchini Japani hadi kufikia hatua ya kuwa na mshindano kwa wanafunzi wa chuo kikuu cha Soka kilichopo nchini humo. Hayo yamesemwa  na Prof. wa chuo hicho Midori Uno wakati akiongea na Mke wa Rais mama Salma Kikwete alipokutana naye katika hoteli ya Intercontinental mjini Yokohama. 
Prof. Uno ambaye ni Mwalimu wa kiswahili katika chuo hicho alisema kuwa hivi Sasa wananchi wengi wa Japani wanakiu ya kujifunza na kuzungumza lugha ya Kiswahili kwani ni rahisi kueleweka. 
 “Katika jitihada zangu za kuwafanya wajapani wengi wajue lugha ya Kiswahili nimetengeneza kamusi ya maneno ya kijapani kuwa ya Kiswahili ambayo watu wengi wanaitumia kwa sasa kwani wengi wajapani wengi wanapenda kujifunza lugha hii”, alisema Prof. Uno. 
 Mashindano hayo ya lugha ya Kiswahili ambayo hufanyika mwezi wa kumi na moja kila mwaka huwa ni ya kuandika na kusoma hotuba ambapo mshindi wa kwanza anapewa cheti, tuzo ya muanzilishi wa chuo hicho, vikombe na zawadi mbalimbali.
 Kwa upande wake Mke wa Rais mama Kikwete alimpongeza profesa huyo kwa jitihada zake za kukuza lugha ya Kiswahili nchini humo na kumuomba aendelee zaidi kufanya hivyo. Alisema kuwa watanzania wanavitu vyao vya kujivunia kama Taifa, moja ya vitu hivyo ni lugha ya Kiswahili ambayo imewaunganisha watanzania wote na kuwa kitu kimoja ndani na n je ya nchi. 
Mama Kikwete alisema, “Ili kumfikia mtu mmoja au watu wengi zaidi ni lazima kuwe na lugha ya mawasiliano hivyo basi nasi tunatumia lugha hii ambayo iliwaunganisha watanzania wote wakaweza kupigania uhuru wa n chi yao kipindi cha mkoloni”. 
Alisema kuwa lugha ya Kiswahili inaongelewa maeneo mengi ya Afrika ya mashariki na ndani ya bara la Afrika na hivi sasa viongozi wa Umoja wa Nchi za Afrika (AU) waliikubali lugha hiyo kuwa lugha ya mawasiliano . 
 Profesa Uno alikuja nchini Tanzania kabla ya kupata uhuru kwa ajili ya kufanya kazi za kujitolea na aliporudi nchini kwake aliamua kuwafundisha wajapani lugha ya Kiswahili pia nchini humo. Redio Japani (NHK) inatangaza matangazo yake kwa lugha ya Kiswahili ambayo ilianzishwa mwaka 1964.
 Mke wa Rais na Mwenyekiti  wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akimkaribisha kwa mazungumzo Profesa Midori Uno, anayefundisha somo la kiswahili kwenye Chuo Kikuu cha Soka kilichoko huko Tokyo nchini Japan. Mama Salma alikutana na mgeni wake huyo kwenye hoteli ya Intercontinental huko Yokohama leo. PICHA NA JOHN  LUKUWI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 03, 2013

    Kiswahili kinakubalika kimataifa,bali watanzania wenyewe tumeshaanza kukitupa kwa kukichanganya na lugha za ajabu ajabu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...