Blog ya Vijimambo ikishirikiana na Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini, Washington, DC, Marekani na Jumuiya ya Watanzania waishio Washington DC, Maryland na Virginia wanapanga kusheherekea miaka 3 ya Vijimambo na kukuletea tamasha ni kuendeleza lugha na utamaduni wa Kiswahili hapa Marekani ili watoto wanaoishi huku waweze kuendeleza matumizi ya lugha hii na utamaduni wake kizazi hadi kizazi. 
Siku ya July 6, 2013  hapa DMV kwenye Hall la Hampton Conference Center lililopo 
207 w Hampton Pl, 
Capitol Height, MD
Mambo mengi yatakuwepo, Vikundi mbalimbali vya utamaduni, Asya Idarous mwanamitindo ya mavazi kutoka Tanzania akishirikiana na hapa Marekani, vyakula vya Kitanzania, Wasanii kutoka nyumbani na hapa Marekani yote ni kudumisha utamaduni wetu wa kiswahili

TEGA SIKIO, HABARI ZAIDI ZITAFUATA
-------------------------------------------------------
kwa wajasiliamali ambao wangepenga kudhamini na kuijipatia meza ya kutangaza bidhaa au shughuli wazifanyazo tafadhali wasiliana 301 613 5165, 301 661 6696 na 301 792 8562 mwisho ni June 15, 2013 Asante
NO COVER CHARGE, FREE DINNER

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Kwanza nawapa hongera Vijimambo kwa kufikisha miaka mitatu. Pili natoa hongera kwa wazo zima la kukienzi ki-Swahili.

    Baada ya kusema hayo, nawajibika kuwashutumu kwa jinsi mlivyoandika tangazo lenu. Kwa nini mnachanganya maneno ya ki-Swahili na ya ki-Ingereza. Je, hiyo ndio namna ya kukienzi ki-Swahili?

    Halafu, kama mngefanya utafiti kidogo kuhusu Mzee Ruksa, mngetambua kuwa huyu ni mwanaharakati wa tangu zamani katika suala la kukikuza na kukienzi ki-Swahili. Mfano ni wadhifa alioshika kama mlezi wa Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA). Msitegemee kuwa Mzee Ruksa ataafiki mlichofanya kwenye hilo tangazo.

    Tafadhalini, bila kuchelewa, badilisheni tangazo hili. Andikeni ki-Swahili sanifu. Tuiheshimu lugha yetu. Ni ishara ya kujiheshimu sisi wenyewe.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...