Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula akimsalimia Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya chama cha PLO, Jehad Abu Znead wakati wa chakula cha jioni alichouandalia ujumbe wa PLO ulipo nchini, kwenye hoteli ya Courtyard jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu wa NEC,
Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro.
Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula akizungumza wakati wa chakula cha jioni alichouandalia ujumbe wa Chama Cha Ukombozi cha Palestina (PLO) kwenye Hotel ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam, Juni 12, 2013. Kushoto ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya PLO, Jehad Abu Znead na Katibu wa NEC ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro na kulia ni Balozi wa Palestina hapa nchini, Dk. Nasri Abujais na Makamu Mwenyekiti wa PLO, Tayseer Khalid.
Makamu Mwenyekiti wa PLO Tayseer akizungumza kwenye chakula hicho.
naona dada hapo kabadilisha shati,from kiss me stupid to looking like a delegate.
ReplyDeleteHuyo maza kweli hajatulia kwali ndani ya mkutano ana-text! Wametoa wapi hawa vimeo! Mjumbe ametumwa na nani huyu mara atavalia 'kiss me stupid' tisheti hapa anatext katika mazungumzo> haya ni maadili gani!
ReplyDeleteHuyu mama jana alikuwa kavaa T-shirt ya Kiss me stupid. Leo wakati wa halfa ya chakula Mwenyeji wake anaongea yeye yupo kwenye messages zake! Ipo kazi hapa!!!!!
ReplyDeleteDah! Apo kazi ipo sivizuri kuona nchi za africa kama sokoni....
ReplyDeleteAlikuwa anaandika yaliyokuwa yanasemwa. Kumbukeni techinolojia, sio kila kitu ni mwendo wa makaratasi tu. Amkeni na msihukumu maana mutahukumiwa.
ReplyDelete