Lango Kuu la kuingilia Banda la Jeshi la Magereza ambapo kuna bidhaa mbalimbali zinapatikana zikiwemo Samani za Ndani, Vifaa vya Ushonaji na Ufumaji, Majiko, Viatu, Vifaa vilivyotengenezwa kwa Mkonge, Mianzi na Henzerani, Vinyago vya aina mbalimbali, Mazao ya Kilimo pamoja na Chumvi. Bidhaa hizo zote zimetengenezwa katika ubora wa hali ya juu na Wafungwa kwa kushirikiana na Askari wa Jeshi la Magereza ndio waliotengeneza bidhaa hizo ambazo zinauzwa kwa bei inayomjali mlaji. Wananchi na Wadau mbalimbali hamna budi kutembelea Banda hili ili kuweza kujionea bidhaa hizo zenye ubora pamoja na kuliunga Mkono Jeshi letu la Magereza katika shughuli na kazi hizo za Mikono ambazo Wafungwa kupitia Programu ya Urekebishaji wa Wafungwa Magerezani Wafungwa hupata ujuzi mbalimbali ukiwa mo ufundi stadi ambao matokeo yake ni bidhaa hizo zilizopo katika Banda la Magereza katika Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa, Saba Saba, Dar es Salaam.
Jiko la Mkaa (Plate mbili) la kuoka Mikate, kuchoma nyama, mishikaki, samaki pamoja na kupikia vyakula mbalimbali. Jiko hili limetengenezwa na Wafungwa wa Gereza Mtego wa Simba , Morogoro kwa kushirikiana na Askari wa Jeshi la Magereza ikiwa ni utekelezaji wa Programu mbalimbali za Urekebishaji wa Wafungwa wanapokuwa wakitumikia vifungo vyao Magerezani kwa kuwapa ujuzi mbalimbali wa ufundi stadi.
Bao la Mchezo wa Jadi ambalo lipo katika Banda la Jeshi la Magereza ambalo lina viti viwili lenye Thamani ya Tsh. 950,000/= bao hilo limetengenezwa na Wafungwa wa Gereza Kuu Ukonga kwa kushirikiana na Askari wa Jeshi la Magereza. Mchezo wa Bao la Jadi ni Maarufu hapa nchini kwani hata Baba wa Taifa, Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere wakati wa uhai wake alipenda Mchezo huo wa Bao la Jadi.
Kitanda cha kulalia chenye ukubwa wa 5 x 6 kikiwa na kiti cha watu wawili na meza havipo pichani. Kitanda hicho kimetengenezwa na Wafungwa wa Gereza Kuu Ukonga kwa kushirikiana na Maofisa Magereza ikiwa ni utekelezaji wa Programu ya Urekebishaji wa Wahalifu Magerezani ili waweze kuwa na ujuzi wanapotoka Magerezani.
Meza ya kujipodolea(Dressing Table) ikiwa na Stuli moja ambayo imetengenezwa kwa kutumia mbao za Mti wa Mkongo yenye Thamani ya Tsh. 1,450,000/= ambayo imetengenezwa na Wafungwa wa Gereza Kuu Ukonga kwa kushirikiana na Maofisa Magereza katika utekelezaji wa Programu ya Urekebishaji wa Wahalifu Magerezani.
Viatu vya aina mbalimbali vinavyotengenezwa kwa kutumia ngozi za wanyama. Viatu hivyo vinatengenezwa katika Kiwanda cha Karanga Moshi cha Jeshi la Magereza pia Wafungwa wa Gereza Karanga kwa kushirikiana na Maofisa wa Magereza wametengeneza Viatu hivyo vyenye ubora wa hali ya juu kama vinavyoonekana.
Muonekano wa Bustani ya mbogamboga iliyopo katika Banda la Jeshi la Magereza lillilopo katika Viwanja vya Sabasaba Jijini Dar es Salaam katika Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa ambayo yameanza leo. Bustani hii inahudumiwa na Wafungwa wa Gereza Kuu Ukonga kwa kushirikiana na Wataalam wa Kilimo wa Jeshi la Magereza ikiwa ni sehemu ya Utekelezaji wa programu ya Urekebishaji wa Wahalifu.
Muonekano wa nje wa Banda la Jeshi la Magereza katika Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa yaliyopo katika Viwanja vya Sabasaba Jijini, Dar es Salaam ambayo yameanza leo (Picha na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 28, 2013

    Kazi nzuri sana Magereza Bao mmelichonga vyema sana!

    Isipokuwa raha ya Mchezo wa Bao kuwe na Mashabiki Pembeni na Marefa kibaooo ambao wao wanaziona sana Kete wakiwa nje ya Mchezo lakini wakiingia ,wanakuwa Vipofu ghafla na Kete hawazioni kabisa wanapapasa mwishowe wanafungwa wanapigwa Supa!

    Sasa hilo Bao hapo juu viti viwili tu vya Wachezaji, Mabenchi ya watazamaji na mashabiki yapo wapi?

    Magereza si mngeweka angalau na Mkeka ama Jamvi Moja kubwa kwa Mashabiki Maandazi wa Mchezo?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 28, 2013

    jiko hilo linauzwa kiasia gani tshillings tuwekeni basi na bei au tuambiyeni wapi tutaweza kulipata nataka nimnunuliye mamsap amechoka kupikia na ma oven etc huku majuu anataka summer time apike na hili jiko so tupeni details wadau

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 28, 2013

    magereza mbona mnauza vitu vyenu kwa bei kubwa sana.Ilitakiwa bei zenu ziwe chini ili wananchi wawaunge mkono kuzinunua,bila hivyo mtauziana wenyewe kwa awamu.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 29, 2013

    kweli tunaona vitu vizuri vya magereza wakati wa maonesho ya sabasaba ,lakini..... there is no way you can see these items anywhere after the sabasaba.
    Halafu, bei zenu hamuwezi kabisa ku- compete dunia ya leo. Kwa mfano bao shs 950,000 is a joke. Labda kama mnataka muuze hilo moja tu kwa raisi akaliweke ikulu.

    Viatu vinavyotengenezwa gereza la Karanga japo havionekani vizuri lakini vina muonekano mzuri. Swali wapi vinapatikana? na, bei yake inaweza kushindana na wauzaji wengine kwenye soko? Je, mtu akiwapa order kubwa mnaweza kuzalisha kwa muda.. au ndio mtaanza kusema hatuna ngozi, gundi, nyuzi? We need to change and to change completely the way we do our things

    ReplyDelete
  5. Hizo bidhaa huruhusiwa kuuzwa au kununuliwa kwa wananchi Wa kawaida? Au husafirishwa kwenda nje direct

    ReplyDelete
  6. Nahitaji jiko la kupika mkate nipe bei na wapi lapatikana 071414200 nijulishe

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...