BONANZA la Maveterani jimbo la Ukonga limefanyika mwishoni mwa wiki na kushuhudia maveterani waalikwa kutoka Sinza timu yenye Star wengi wa zamani ya Golden Bush wakiibuka mabingwa wa mchezo wa Soka.

Bonanza hilo lililoandaliwa na Mbunge wa Jimbo hilo Eugene Mwaiposa lilizikutanisha timu zipatazo kumi za jimbo hilo na timu mbili zilialikwa kwenye Bonanza hilo.

Ushindani kwenye michuano hiyo ulikuwa mkali ambapo wenyeji wa mashindano hayo timu ya Pugu ilitinga fainali na kupambana na timu ya Golden Bush ya Sinza iliyojaza nyota kama Salum Sued Kusi, Abuu Mtiro na Amani Simba.

Hata hivyo haikuwa kazi rahisi kwa mastaa hao kupata ubingwa huo kwa vijana wa pugu hadi pale ilipofikia changamoto ya mikwaju ya Penalt 5, ambapo Golden Bush walipata Penalt saba kwa 6, kutokana na kumaliza muda wote wa mchezo bila kufungana.

Kivutio kikubwa kwenye bonanza hilo kulikuwa kwa mwanamuziki wa kizazi kipya KR Mulla, alipoingia kwa upande wa timu ya Golden Bush na kufanikiwa kuunganisha kross kali na kupiga bao ambapo alishangalia kwa Staili ya mapanga Shaa! na kurusha miguu juu.
Mbunge wa jimbo la Ukonga Eugene Mwaiposa akimkabidhi jezi kapteni wa timu ya vijana wa CCM wa jimbo hilo Abubakari (fulana ya bluu) wakati walipoalikwa kwenye bonanza la maveterani wa jimbo hilo.
Mbunge wa Jimbo la Ukonga Eugene Mwaiposa akikagua timu za Kigogofresh na Tumaini kabla ya kuanza kwa mpambano wao kwenye bonanza la Maveterani lililoandaliwa na mbunge huyo mwishoni mwa wiki eneo la Pugu Kajiungeni jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, matokeo ya mchezo huo Kigogo ilishinda 2 kwa 1.
Wazee wakichuana vikali kumkimbiza kuku.
Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Bombani Pugu akishangilia mara baada ya kukamata kuku aliyeshindaniwa na Wazee wa eneo hilo ikiwa ni miongoni mwa michezo iliyofanyika kwenye bonanza lililoandaliwa na mbunge wa jimbo la Ukonga Eugene Mwaiposa mwishoni mwa wiki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 24, 2013

    PENDEKEZO LA ZIADA KTK KATIBA:

    Mbio za kufukuza Majogoo iwekwe Kikatiba kuwa ndio Mchezo kwa ajili ya Waheshimwa Wabunge ili kuwaweka ktk afya njema na kupunguza nundu zao!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 24, 2013

    nafikiri haya mambo mengine ya kujifurahisha nafsi zetu kwa kutesa wanyama haipendezi , huyu kuku maskini anakimbia sio kwa kufurahia mchezo , bali kwa hofu ya maisha yake , jee mmoja wetu atakuwa tayari kutiwa hofu kama hivyo halafu tuiite ni mchezo? naomba ufafanuzi

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 25, 2013

    Hahahahahahaha hahahahha hahahah du pendekezo zuri sana mdau.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 25, 2013

    KWANI HUJAONA NGOMBE NA FARASI AKIKIMBIZWA NA KUKIMBIA NAO NI MCHEZO MAARUFU WACHENI UJUNGA WATANZANIA,

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...