Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu (CCM), akihutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Shule ya Azimio, Tandika, Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. Mtemvu alivikabidhi vikundi vitano vya Kuweka na Kukopa (VICOBA, kila kimoja msaada wa sh. 500,000 na kikundi cha ulinzi shsirikishi sh. 500,000 za kutunisha mifuko hiyo.
Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu (kulia), akikumbatiana na mmoja wa wanachama wa kikundi cha Vicoba cha Tuyangatane waliofurahi kupatiwa msaada wa sh. 500,000 za kutunisha mfuko wa kikundi hicho.
Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu (CCM), wa pili kulia, akimpatia cheti Mwanaisha Gea ambaye amekuwa miongoni mwa vijana 56 waliohitimu mafunzo ya Ulinzi Shirikishi, katika mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Shule ya Azimio, Tandika, Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. Mtemvu alikikabidhi pia kikundi hicho cha Ulinzi Shirikishi sh. 500,000 za kuanzishia Saccos yao. Kulia ni Diwani wa Kata ya Azimio, Hamis Mzuzuri.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...