Miss Tabata 2013 Dorice Mollel (22) yupo nchini Ujerumani kwa ziara ya wiki tatu ya kudumisha ushirikiano kati ya nchi hiyo na Tanzania. 
Dorice ambaye ni mwanafuzi wa mwaka wa pili katika chuo cha Kumbumbumbu ya Mwalimu Nyerere ni mmoja ya wanafuzi 10 kutoka nchini waliyochaguliwa kwenda mjini Hamburg na Berlin kudumisha ushirikano na kujifunza tamaduni za Kijerumani.
 Mratibu wa Miss Tabata, Joseph Kapinga amesema  jijini Dar es Salaam kuwa ziara hiyo imedhaminiwa na MitOst Hamburg ya Ujerumani na Tanzania Youth Coalition.
 “Tunashukuru sana hii ni nafasi pekee kwa Dorice kujifunza mambo mengi kabla ya kushiriki kwenye shindano la Miss Ilala ambayo yamepangwa kufanyika Agosti. 
Tunaimani ziara hii itapanua mawazo yake na atakuwa tishio kwenye shindano hilo la urembo,” alisema Kapinga. Dorice ambaye alishinda taji la Miss Tabata Mei 31, aliondoka nchini Juni 6 na atarejea Julai 5.
Dorice akiwasili Hamburg
Dorice akiwa katika matembezi


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...