Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania,
MKURABITA, unaendelea na utekelezaji kwa vitendo, wa awamu ya kwanza
ya kuwapatia “Maisha Bora kwa Kila Mtanzania” kwa kuendelea kugawa
hati miliki za kimila kwa wanavijini mbali mbali, ili kwanza
kuwamilikisha rasilimali, kasha ndipo kuwaelimisha jinsi ya kuzitumia
rasilimali hizo kujiletea maendeleo ambayo ndiyo yatakayo leta maisha
bora kwa kila Mtanzania.
Hayo yamebainishwa na Mratibu wa Mkurabita, Bibi. Seraphia Mgembe,
wakati akitoa tathmini ya zoezi la kuwakabidhi hati miliki za kimila,
kwa wakulima wa zao la chai wa wilaya ya Mbinga, Mufindi na Njombe,
lililohotimishwa hivi karibuni.
Bibi Mgembe amesema, maisha bora kwa kila Mtanzania, haya patikana kwa
wananchi kubweteka na kuisubiria serikali ndio ifanye kila kitu, bali
ni kwa serikali kujenga mazingira ya uzalishaji mali, ikiwemo
kuwamilikisha wananchi rasilimali zao, na maendeleo ya kweli,
yatapatikana kwa wananchi kuelimishwa na kujibiidisha katika kutumia
rasilimali hizo kama dhamana za kupatia mitaji ya kujiletea maendeleo.
Bibi Mgembe amesema, huku zoezi la kuwamilikisha wananchi rasilimali
zao likiendelea, MKURABITA inayapitia tena yale maeneo ambayo tayari
wananchi wake wameisha kabidhiwa hati miliki, ili kuwajengea uwezo
wananchi hao, jinsi ya kuzitumia hati miliki hizo kama dhamana na
kukopa katika mabenki ili kutumia fedha za mkopo kujiletea maendeleo.
Bibi Mgembe amesisitiza, maendeleo ya kweli na endelevu, ni yale
yanayotokana na matumizi ya rasilimali zilizowazungunguka wananchi
husika, nan i kwa kulitambua hilo, ndio maana MKURABITA imekuwa
ikizishirikisha taasisi za kifedha, ili kuwaelimisha wananchi fursa
mbalimbali za mikopo ya kibiashara na kimaendeleo zinazoweza
kupatikana kwa kutumia dhamana za hati miliki zao.
Kwa upande wao, Wakuu wa wilaya za Njombe, Bi. Sarah Dumba na Mkuu wa
Mufindi, Bi. Evarista Kalalu, waliipongeza MKURABITA kwa juhudi zake
za kuhakikisha wakulima wa chai sasa wanayamiliki rasmi mashamba yao
ya chai, ambapo mwanzo walikuwa na utajiri ambao hauwafaidii chochote
zaidi ya kulima na kuuza mazao yao, lakini sasa, sio tuu ni wamiliki
wa mashamba hayo, bali wanaweza kuzitumia hati miliki zao, kukopa
mikopo mikubwa ya kimaendeleo.
Jumla ya hati miliki za kimila zaidi ya 2000 zilikabidhiwa kwa wakulima wa chai.
Wananchi wa Njombe, wakifurahia kukabidhiwa hati miliki za kimila,
kulikofanywa na MKURABITA hivi karibuni.
Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Sarah Dumba, akimkabidhi hati miliki ya
kimila, Mwanakijiji wa kijiji cha Matembwe, Bw. Solomon Matunasa
wakati wa hafla fupi ya MKURABITA kukabidhi hati miliki za kimila kwa
wakulima wa chai wa Rungwe, Mfindi na Njombe hivi karibuni. Katikati
ni Mratibu wa MKURABITA, Bibi Seraphia Mgembe.
Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Sarah Dumba, akimkabidhi hati miliki ya
kimila, Mwanakijiji wa kijiji cha Iwafi, Bw. Eneas Paruasi wakati wa
hafla fupi ya MKURABITA kukabidhi hati miliki za kimila kwa wakulima
wa chai wa Rungwe, Mfindi na Njombe hivi karibuni. Katikati ni Mratibu
wa MKURABITA, Bibi Seraphia Mgembe.
Ivi yule Tuntemeke Sanga mwenye DEGREE saba yupo???
ReplyDelete