Mwenyekiti wa chama kikuu cha ushirika mkoa wa Kilimanjaro(KNCU)Maynad
Swai akitoa taarifa kwenye mkutano mkuu wa chama hicho unaofanyika
katika ukumbi wa Hotel ya KNCU ulioo mjini Moshi.
Kaimu mrajisi wa vyama vya ushirika nchini Bw Peter Rutabanzibwa akizungumza katika mkutano mkuu wa chama cha ushirika mkoa wa Kilimanjaro KNCU.
Wajumbe wa mkutano mkuu wa chama kikuu cha ushirika mkoa wa
Kilimanjaro wakifuatilia kwa makini maelezo ya mwenyekiti(hayupo
pichani).
Mjumbe akichangia hoja katika mkutano huo.
Baadhi ya vingozi wa KNCU katika mkutano huo.
Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii Moshi
Serikali inawasiliana na benki kuu ili kuweka mipango madhubuti ya
kuziimarisha na kuziendeleza benki za ushirika nchini ili kuzijengea
uwezo wa kuwahudumia wakulima kwa kuvipa mikopo vyama vikuu vya
ushirika badala ya kuzitegemea taasisi nyingine za fedha.
Kaimu mrajisi wa vyama vya ushirika nchini Bw Peter Rutabanzibwa
amesema hayo katika mkutano mkuu wa chama kikuu cha ushirika mkoani
kilimanjaro (KNCU) baada ya wajumbe wake kueleza kutoridhiswha kwake
na utendaji wa benki ya ushirika mkoani humo ya kilimanjaro
co-operative bank(KCBL).
Bw Rutabanzibwa amesema, lengo la serikali ni kuhakikisha kuwa benki
hizo ikiwemo ya kilimanjaro zinafikiwa kiwango cha juu katika
kuwahudumia wakulima hivyo jukumu la wanachama wa vyama vyote vya
ushirika nchini na kuziunga mkono benki hizo.
Hata hivyo baadhi ya wajumbe wa mkutano huo walieleza kutoridhishwa
kwao na mwenendo wa benki hiyo ambayo imekuwa ikifanya semina za
kuvishawishi vyama vya msingi vya ushirika vijitenge na kncu katika
biashara ya kahawa na kuuvuruga ushirika.
Kutokana na hali hiyo mwenyekiti wa KNCU Bw Maynard Swai ameutaka
mkutano huo utoe tamko juu ya benki hiyo kutaka kuusambaratisha
ushirika na kupendekeza wajumbe wawili wa bodi ya wakurugenzi wa KNCU
waingie kwenye bodi ya wakurugenzi ya benki hiyo ili kudhiti hali
hiyo.
Katika taarifa yake mwenyekiti wa kncu Bw Swai amesema, chama hicho
kimeimarisha mtaji wa benki hiyo kwa kuipatia zaidi ya shs. 153.6mil/=
kutokana na kilo 1,536,340 za kahawa iliyokusanywa kutoka vyama vya
msingi vya ushirika na kuuzwa kwa msimu wa 2009/2010.
KNCU!
ReplyDeleteKwa anguko la kilimo cha kahawa mkoani Kilimanjaro,KNCU inajivunia lipi?
Je mna mikakati gani ya kufufua zao hili? ama nguvu zaidi sasa ziko ktk benki na hiyo hospitali ya rufaa mnayotaka kuanzisha.
Shame on you KNCU!