Mshindi wa shindano la BE FORWARD PHOTO CONTEST ambaye ni mwanafunzi wa chuo kikuu cha Makerere nchini Uganda,Bwa.Sunday Robert akifanya mahojiano mafupi mbele ya wanahabari kutoka vyombo mbalimbali,namna alivyojishindia gari aina ya Landcruiser Prado kupitia shindano hilo la mtandao wa kijamii wa facebook.
Meneja mauzo wa kampuni ya BE FORWARD .JP ambao ni wasafirishaji wa magari kutoka Japan kwenda nchi mbalimbali,Bwa.Eiichi Mizuyama akimkabidhi Bwa.Sunday Robert mfano wa funguo mara baada ya kujishindia gari aina ya Landcruiser Prado kupitia shindano hilo la BE FORWARD PHOTO CONTEST lililofanyika kwa njia ya Mtandao wa kijamii wa facebook.
Bwa. Eiichi Mizuyama alisema kuwa pamoja na kumpata mshindi huyo wataendelea kufanya shindano hilo na kuwapata washindi wengine,katika suala zima la kuhakikisha kampuni hiyo ya BE FORWARD .JP inaendelea kuwajali wateja wake kwa namna mbalimbali,ikiwemo na suala la zima la umakini mkubwa katika kusafirisha bidhaa zao zikiwa salama mpaka mlangoni kwa mteja wao.
Bwa. Eiichi ameeleza kuwa pamoja na kuwa kampuni hiyo makao yake yako Japan,lakini pia wamefungua tawi la kampuni hiyo hapa nchini katika suala zima la kuwahudumia wateja watakaokuwa wanahitaji huduma zao za uhakika.
JAMANI, JAMANI, SIO MAKELELE; NI MAKERERE!
ReplyDeleteDah, waandishi wa hii blog jamani hata kuandika MAKERERE imekuwa taabu? Haileti picha nzuri kushindwa hata kuandika jina la mahali sawasawa. Siyo MAKELELE jamani...
ReplyDeleteDuuh, ama kweli Kiswahili kimekwisha....
ReplyDeleteMakelele ndio wapi tena??
Jamani kazeni ulimi. Matamshi ya "R" mbona mtihani Bongo siku hizi??
Ni Chuo cha MAKERERE.....
Jamani ni Makerere
ReplyDeleteNi Makerere
ReplyDeleteThis is getting a bit stupid, ? Makelele, what????????, it should be MAKERERE, Michuzi ajiri watu wenye alau kadiploma ka uandishi wa habari,unajiaribia jina kwa uandishi huu uchwala!
ReplyDeleteNa wewe Pia, siyo uchwala ni uchwara
DeleteNa wewe Pia, siyo uchwala ni uchwara
DeleteMakelele?au Makerere?
ReplyDeleteJAMANI WATANZANIA WENZETU??????????MBONA MNAHARIBU KISWAHILI?WHAT THE MEANING OF MAKELELE?NI MAKERERE PLEASE.
ReplyDelete