Taifa Stars ambayo inatupa karata yake ya pili ugenini kwenye mechi za mchujo za Kombe la Dunia dhidi ya Morocco (Lions of the Atlas) kwenye Uwanja wa Grand Stade jijini Marrakech, Morocco, imefungwa hadi bao 2-1 na mpira umekwisha.
Awali Taifa Stars Ilipoteza mchezo wa kwanza ugenini dhidi ya Ivory Coast mwaka jana, na kushinda mbili mfululizo nyumbani dhidi ya Gambia na Morocco. Mechi ya leo ni ya pili kwa Stars katika uwanja huo ambapo mwaka juzi ilifungwa mabao 3-1.
Tanzania wamecheza vizuri zaidi kipindi cha pili walipokuwa na watu kumi baada ya mmoja kutolewa na kadi nyekundu.Muda umefika wa kutafutiwa mechi za kirafiki na timu zinazoeleweka sio kucheza na Sudan.Watafute mechi za kirafiki kwenye nchi za ulaya na itawasaidia wachezaji waonekana na wanunuliwe kuja kucheza kwenye ligi za Ulaya n.k.Kama kutakuwa na mikakati mizuri Tanzania itafika mbali sana.Ila safari ya Brazil imeishia hapa hawawezi kuwafunga Ivory Coast na hata Morocco hawawezi kuwafunga Ivory Coast,kwenye hili kundi ni Ivory Coast watasonga mbele.
ReplyDeleteMtoto wa Kabwela,Sweden
Napenda kutoa pongezi zangu za dhati kwa timu Tanzania kwa kuanzia, mwalimu, wachezaji na viongozi wao wote.Hakika hii ni mara yangu ya kwanza kuona timu ya taifa ikicheza, kwakweli wanastahili kila aina ya pongezi, wameonesha kiwango kikubwa mnoo na profesheno,kila mchezaji amecheza vizuri na kwa umahili mkubwa.Hongera stars. Sina hakika kama ile penati ya jamaa ni halali pamoja na adhabu ya kutolewa aliyopata mchezaji wetu.
ReplyDeleteNaona hawa ndugu zangu wawili hapo juu tulikuwa labda tunaangalia mpira tofauti. Timu haijacheza vizuri na ndiyo maana tumefungwa msilete uzalendo ambapo hapastahili. Leo tungelala hata bao sita kama wale Morocco na wenyewe wangekuwa vizuri. Timu zote zilikuwa na mapungufu makubwa ya kiufundi na kibinafsi kwa wachezaji. Mchezaji uko kwenye kaunta attack unaanza kuangalia nyuma kwanza hiyo inaonyesha kutojiamini kwa wachezaji wetu. Pili defence haielewani kabisa kuna makosa madogo madogo lakini yana madhara makubwa kwa hili naweza kusema kuna mapungufu ya uzoefu. Kupigiana pasi mtu anasubiri mpaka adui anajipanga ndiyo atoe pasi ambayo inaonyesha kabisa amepiga tu basi lakini moyoni mwake anajua haitamfikia mlengwa. Umaliziaji pale mbele ni mbovu kabisa hatuna strike ambaye ni wembe mwenye jicho na goli siyo hawa wakupiga tu shuti golini ambalo halina hata ufundi tutasubiri sana kwa mpira ule. Kocha mmoja tu hatoshi kuinoa taifa stars. Tunahitaji kocha wa maforward na defence hayo maeneo yasukwe kiufundi siyo ndolela ndolela tu.
ReplyDeleteTaifa Stars wamecheza kwa ujasiri tu lakini siyo kama football timu wale wanaojua mpira watajua nimeongea nini. Ahsanteni
Naipongeza sana stars kwa kazi nzuri ya kishujaa kwani wlipigana kiume pongezi nyingi sana ziende kwa coch mkuu wa stars Kim kwani amefanya kazi kubwa sana kama amezaliwa bongo Uzalendo!!!!! keep it up kim and all stars!BUT MAONI YANGU NI KWAMBA LAZIMA CHAMA CHA MPIRA CHA TANZANIA KIWAKILISHE RUFAA YA YA VITENDO VYA MAKUSUDI NYA KINYAMA WALIVYO FANYIWA TIMU YETU YA STARS,KWA KUKATALIWA KUINGIA NDANI YA UWANJA KUFANYA MAZOEZI KUZIMIWA TAA YA WAKATI WA MAZOEZI, HII NI MBAYA SANA NA NDIO MAANA PAMOJA NAKUWA NA JINA KUBWA KISOKA LAKINI KUTOKANA NA UFINYU WALIONAO WA KUFIKILI HUWA HAWAFIKI KOKOTE! MAONI YANGU NI KWAMBA UMEFIKIA WAKATI WA KUTO WALEMAZA HAWA JAMAA NA MBINU ZAO ZA KISHENZI, CHAMA CHA MPILA CHA TANZANIA LAZIMA KIFIKIRIE HILI HIKIWEZAKANA KUKATA RUFAA ILI HATUA KALI ZA NIDHAMU NDANI YA SOKA ZICHULIWE!!!!!!!!!
ReplyDeletemdau kutoka Norway!!!!!!!!!!
Binafsi sikutegemea kwamba tungewashinda Morocco kwao lkn hata hivyo hongera kwa hatua tuliyofikia. Jambo moja ni kwamba ushindi ni ushindi tu kushindwa ni kushindwa tu kuwe kwa taabu au kwa mteremko!!!
ReplyDelete