Warembo 11 kati ya 12 wanaopanda jukwaani leo kuwania Taji lenye Sifa Kuu mbili ya Redd's Miss Sinza 2013, lakini pia linaloshikiliwa na Redd's Miss Tanzania 2012-2013, Brigit Alfred, leo katika Ukumbi wa Meeda Club uliopo Sinza Mori. Katika shindano hilo litakalosindikizwa na burudani kabambe kutoka kwa Bendi mahiri ya African Stars, 'Twanga Pepeta', viingilii vitakuwa ni Sh. 20,000/= kwa VIP na Sh. 10,000/= kwa viti vya kawaida. Shindano hili limedhaminiwa na Redds Original, Mtandao wa Sufianimafoto Blog, Dodoma Wine, Chilly Willy Energy Drink, Fredito Entertainment, CXC Africa, Clouds Media Group na Salut5.com.
Hapa wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa mazoezi yao....ya maandalizi.... Picha na www.sufianimafoto.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 07, 2013

    Kwanza jinsi walivyokaa hawana adabu. Mtoto wa kike uliyeleleka utakaaje hivyo? Au na kuonyesha sehemu za siri ni aina ya mashindano?

    Watz tumefika pabaya

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 07, 2013

    Za mtumbani zimekubali!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 07, 2013

    Mshindi wa vigogo....... au? Mnapoteza maadili wenyewe,halafu mnahamaki eti utamaduni unapotea:

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...