Taarifa zilizopatikana mapema leo asubuhi,zinaeleza kuwa Mume wa Mwanamuziki Mkongwe wa Miondoko ya Taarab,Malkia wa Mipasho,Bi. Khadija Kopa, aitwaye Jaffari Ally amefariki dunia usiku wa kuamkia leo majira ya saa 9 usiku.

Taarifa za kuthibitika juu ya msiba huo,zimetolewa na Katibu wa Bendi ya TOT,Gasper Tumaini.

Taarifa za awali zilieleza kwamba chanzo cha kifo chake ni ugonjwa wa Malaria, ambapo siku ya Jumatatu marehemu Ally alipelekwa Hospitali ya Lugalo kwa ajili ya kupata matibabu.

Taarifa zaidi zinasema kwamba marehemu alipata nafuu na kurudi nyumbani kwao Bagamoyo, hali ambayo ilimpelekea Khadija Kopa kusafiri kikazi, na inasemekana mpaka umauti unamkuta Jaffari, Mkewe Khadija Kopa alikuwa yupo kikazi mikoani kwa ajili ya shughuli zake za kimuziki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

 1. AnonymousJune 06, 2013

  pole sana wafiwa kwa msiba huu mzito kwa Familia hizi

  ReplyDelete
 2. AnonymousJune 06, 2013

  inna lillahi wa inna ilayhi rajiun, Muumba amrehemu. Tuliyebakia nyuma tujiandae kwa kuwa nasi tutatamkiwa mfu muda wowote na kwenda kuoanana na Aliyekuumba.

  ReplyDelete
 3. AnonymousJune 06, 2013

  haya matatizo ya madaktari wa bongo wanakupa dawa za malaria bila hata kujua kama unamatatizo gani mengine ambayo yataleta reaction mbaya kwa mgonjwa

  ReplyDelete
 4. AnonymousJune 07, 2013

  RIP


  MEGGIE IMPOSTRA

  ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...