Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji Msanii wa taarabu Hadija Koppa nyumbani kwake mjini Bagamoyo jana kufuatia kifo cha Mumwewe Marehemu Jaffari Ali Yusuf aliyefariki na kuzikwa wiki iliyopita.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiifariji familia na ndugu jamaa wa msanii maarufu wa taarabu na mjumbe wa Halmashauri kuu taifa CCM Hadija Koppa kufuatia kifo cha mumwewe Jaffari Ali Yusuf kilichotokea wiki iliyopita na kuzikwa jijini Dar es Salaam.Wa pili kushoto ni Waziri wa Elimu Dkt Shukuru Kawambwa na wa pili kulia ni Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Mhe. Ahmed Kipozi na kulia ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM Ndugu Ridhwani Kikwete. Picha na Freddy Maro
Mh. Ahmed Kipozi! ni yule aliyekuwa mtangazaji?
ReplyDeleteOhh, sasa ngoja nami nijipange walau awamu ijayo "Nilambe hizi post"
Poleni kwa msiba.
ndiye huyu huyu kipozi unayemfahamu.Ila jipange maana kuna katiba mpya inakuja na pia raisi ajaye si mtu wa huruma huruma za kuwapa watu madaraka.
ReplyDeleteAhmed Kipozi ndio huyo huyo wa RTD.
ReplyDeleteJamani mimi tangu nakua namsikia Hadija KoPA, yaani miaka yote hiyo ya uimbaji ndo nyumba yake iko hivyo!!! jama ni kwa kinara km huyo alitakiwa kuwa na mansion. Mh kama mambo ndo hivyo ni bora kufanya kazi zingine na sio uimbaji/usanii Africa, loh!
ReplyDelete